Saturday, 22 March 2014

Je tumshukuru au kumuandama Kikwete kutupa Katiba mpya?


Kwa hali ilivyo ni kwamba CCM watatufanyia unyani na kutuletea "Katiba Mpya" kwa maana tofauti. Badala ya kutegemea Katiba Mpya nadhani tutegemee kitabu kipya chenye kubeba mambo yale yale ya zamani. Kwa hotuba ya juzi ya mwenyekiti wa CCM rais Jakaya Kikwete ni kwamba hakuna kitu kinachoitwa Katiba Mpya. Kama ipo basi ni ya zamani kupitia njia mpya ya kuunda tume ambayo hata hivyo Kikwete aliizodoa na kuidhalilisha huku akijitia mtalaam aliyeishiwa kuumbuka hasa alipojaribu mambo kama takwimu. With this monkey business Tanzanians need to fast and weep.

4 comments:

Anonymous said...

Mimi napingana na zoezi hili kuwa na Katiba mpya ndiyo jibu pekee la matatizo na changamoto. Sababu hata katiba iliyopo haijawahi kutekelezwa yale yote yaliopo zaidi tumekuwa tukichagua vipengele ambavyo vinavyotunufahisha sisi binafsi badala umma ndiyo ufaidike. Kimsingi mambo yanayotusumbua siyo tuu Katiba, Tumekosa Uzalendo, Utawala wa sheria, Kujituma na kuwajibika bila kikomo

NN Mhango said...

Anon,
Umesema vyema na umeskika. Naamini wengine watakusoma na kuja na mengine zaidi. Ni kweli uzalendo kwetu umeyeyuka hasa ambapo sasa kila mtu anajihudumia na tunashindana kutafuta makuwadi wa kuwauzia raslimali na watu wetu. Ni balaa na aibu.

Anonymous said...

Ni ajabu mno kwa katiba ambayo haijawahi kuheshimiwa hata siku moja kuonekana eti ni kikwazo na ina kero!! Wanasiasa hawa wanatuchukua tu just for a ride, kwa kweli.

Hapa yawezekana kuna uhuni unaotakiwa kuhalalishwa (na hiyo mpya). Hapo ndiyo waTanzania wa sasa na wajao watakoma zaidi ya hali ilivyo sasa.

Jaribu said...

Nakuunga mkono, Anonymous. Waswahili huwa tunafikiria kila kitu kina njia ya mkato. Tukitaka maendeleo, katiba mpya, ukitaka utajiri, uchune mtu ngozi au uibe serikalini. Ingawa katiba inahitajika, lakini hata hii katiba ya sasa hivi hairuhusu wizi, unyanyasaji na madudu mengine. Halafu shida yenyewe tunagemea huruma za hao hao wezi na majambazi kutupa katiba mpya. Ni kama Colombia kutegemea Pablo Escobar awape katiba mpya.