Thursday, 13 March 2014

Mnamkumbua master Sergeant Samuel Kanyon Doe rais wa zamani wa Liberia?

Kwa wale ambao hawakubahatika kuona jinsi uovu usivyolipa, nawaletea video ya mateso ya Samuel Kanyon Doe aliyesifika kwa wendawazimu na tamaa ya madaraka asijue malipo ni hapa hapa duniani. Naomba msamaha kutokana na taste ya kila kitu ila huo ndiyo ukweli. Si vibaya kusikia muziku mkubwa alioimbishwa mbweha huyu aliyejiona ni mali kuliko wengine asijue madaraka ni mapito na cheo ni dhamana. Je unapata somo gani?

5 comments:

Anonymous said...

waafrika ni waoga
North Afrika waarabu wanaweza
Nguvu ya umma inaleta mabadiliko
Watanzania maneno mengi na waoga kutetea haki zao
Jifunzeni toka Ukraine

NN Mhango said...

Anon,
Sikubaliani nawe. Hawa waliomuua kwa kumsulubu Doe ni waswahili wa kawaida tena bila kusaidiwa na CIA kama ilivyokuwa kwa akina Gaddafi na Saaddam Hussein. Kinachogomba ni mfumo uliowalea wahusika. Kwa Tanzania nadhani tatizo ni mfumo na si watanzania. Hayo ndiyo maoni yangu.

Anonymous said...

Mwl Mhango naona akina Mjengwa aka vuvuzela wameishadandia hii thread na kujifanya wanaijua sana historia.

Jaribu said...

Siyo kama hawaioni, lakini watakuja na ngonjera yao ya amani na utulivu wakati wanatuibia na kutufukarisha. Doe naye alikuwa anajiona "invincible', lakini hivi ndio alivyoishia. Sidhani hawa madakta njaa wana uwezo wa kutafakari.

NN Mhango said...

Sijui kama kwa kizazi hiki watafanikiwa. Zamani angalau kulikuwa na vitu vya kudanganyia kama elimu na huduma za afya za bure chini ya Mwalimu. Kwa sasa vijana hasa wamepigika Mungu mwenyewe anajua. Natamani wahusika waone mwanga waache kufikiri kwa massaburi na matumbo yao. Ni hatari.