The Chant of Savant

Sunday 13 March 2016

Wakuu "wapya" wa mikoa, Magufuli achemsha

Ukiangalia orodha ya walioteuliwa kuwa wakuu wapya wa mikoa unashangaa kama imeandaliwa na Jakaya Kikwete au John Magufuli. Maana, hakuna jipya zaidi ya muendelezo wa usanii ule ule. Hapa ndipo alichokificha Magufuli kitafichuka kirahisi. Amerejesha ujeshi, u-CCM, ukale, kujuana na kila aina ya kufadhiliana na kulindana kwenye uteuzi wake mpya usio na upya wowote. Hivi watu kama Makala, Killango-Malecela wamerejeshwa na nini pamoja na kushindwa kwenye kura za maoni zaidi ya kufadhiliana na kulindana kichama? Uhovyo wa Magufuli hauishii hapo. Rejea anavyofanya mambo kibabe na kizamani bila kufuata sheria. Mfano, hadi sasa watanzania wengi wameishaanza kustukia udaktari wake na kiingereza chake broken ukiachia mbali kutoa maelekezo kana kwamba Tanzania ni mali yake binafsi. Rejea Magufuli alivyowaambia Bank of Tanzania (BoT) wafute majina ya wafanyakazi hewa badala ya kutaka wafikishwe mahakamani. Hata hiyo expose yake inatia shaka kama ni kweli au kanyabwoya.
Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

4 comments:

Anonymous said...

Mwalimu Mhango.
Kusema kweli hili la BoT hata nami niliachwa na maswali kuliko majibu kwa utaratibu wa Magufuli ktk utekelezaji wake wa kazi kwa nn aagize kufutwa majina hewa?Kwa nini asiwatafute wale ambao wameaajiri majina hayo hewa na hatimae hayatumbue majipu yao?Na hili la kwamba uwenda kumelipwa madeni hewa,je ukweli wake ni upi?kwa nini tusilijue hili kama serikali imelipa madeni hewa na kama madeni hewa ni kiasi gani?Au BoT kwa vile kulijulikana ni pango la watoto wa vigogo ndio imemfanya Magufuli agwaye kuchukua hatua zinazostahiki ili kuwaridhisha vigogo wa watatoto hao?Tungemshauri rais wetu asiwe na utaratibu wa kuwa na kuidanganya mizani mzani mmoja anaupima kwa makini na usahihi kwa viongozi wasiokingiwa vifua na mizani mingine akaipunja kwa viongozi ambao wanaokingiwa vifua na hili la BoT ni mfano hai.Kama kutumbua majibu yatumbuliwe yote bila kujali ni majbu uchungu,majibu usaha,na majipu maji yote ni majipu tu na yanahitaji kutumbuliwa.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon nakubaliana nao. Kuna uwezekano Magufuli amewagwaya akina Mkapa na Mwinyi wenye watoto wao BoT. Nadhani anabembeleza apewe uenyekiti wa CCM awageuzie kibao au naye aishie kuwa kama wao. Si unajua tena CCM. Maagizo yake ya kuwasahidia wahalifu yameanza kumshushia imani na heshima hasa kwa watu makini.

Anonymous said...

Mwalimu Mhango,kuhusu hili la wakuu wa mikoa je isiwe tu kutaka kuwaridhisha baadhi ya watu hususa wale ambao wamechangia kwa ainq moja au nyingine ya karibu au ya mbali kumuweka madarakani japo kwamba walilazimika kufanya hivyo baada ya kuona kwamba kwa upande wa upinzani wanaweza kuichukua nchi?Kuna tuhuma nyingine imejitokeza dhidi yake kwamba orodha ya majina ya wakuu hao wa mikoa wengi wao ni wafuasi wa dini ya kikristo ikikuwa ni kweli kiitikadi na matendo au ni kwa kusikika kimajina tu na hatiae kutuhumiwa rais wetu kwamba ni mdini,kwa hili mimi naweza kumtetea kwani kumtuhumu Magufuli kwamba ni mdini ni mgando wa akili ambao unagandishwa na jazba za kidini na ni kumdhulumu Magufuli kwa tuhuma hiyo kama walivyomdhulumu Mwalimu Nyerere.

Na wale wenye nia mbaya na nchi ma kwa magufuli wanaweza kuitumia karata hiyo ya udini kwa kulichafua jina lake na watanzania baada ya kuyasghulikia mambo muhimu na kushirikiana na rais wetu katika kuleta maendeleo na mabadiko ya nchi na wananchi, nchi ambayo na wananchi ambao walikuwa katika cbumba cha intensive care kwa miaka yote 30 iliyopita.Tunachotaka ni nani ana uwezo wa kuihudumia nchi na wananchi kama ipasavyo bila ya kujali dini yake, kabila lake na zone yake,lakini tukianza kudai kwamba mikoba ya uongozi tuigawe kutokana na asilimia ya dini za watanzania itakuwa ni mwanzo wa kujichimbia kaburi la kuzikwa kwa pamoja na tukianza madai hayo hatimae tutafikia kuanza kudai kwamba viongozi watokane na dini zao,zone zao na kabila zao.Mwalimu Nyerere alishatujengea misingi na imara ya amani kwa nchi na kuepukana na udini na ukabila.Na tumalizie tu tukisema viongozi wanapokuwa madarakani wanawahudumia wanachi wa Tanzania na wala hawawahudumii wakristo au waisilamu na ikumbukwe tu zaidi wananchi wa tanzania walipokuwa wanateseka katika miako yote 30 ilyopita walikuwa ni wakristo na waisilamu chini ya uongozi wa maraisi wenye dini za kikristo na kiisilamu na zibaki dini makanisani na misikitini waumini wa dini hizo wakitoka makanisani na misikitini mwao jambo la kwanza la kulipa umuhimu ni TANZANIA KWANZA.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo yana mashiko sana. Wanaoingiza udini kwenye uteuzi wanapaswa kukumbushwa mambo makubwa mawili. Kwanza, Magufuli hakuchaguliwa kwa misingi ya dini wala kutakiwa kufuata diktat ya dini yoyote. Pili wanaoona dini au jinsia havijatendewa haki wanapaswa kusoma katiba ili kujua kuwa hakuna hata sehemu moja inayomtaka afuate itikadi zaidi ya sera alizoahidia na kuapa kutekeleza. Hivyo, kwangu madai ya udini haya mashiko zaidi ya kuwa harakati mfu na kutapatapa. Tunachopaswa kufanya hapa si kujificha kwenye udini. Tumuhukumu na kumkosoa Magufuli kwa kuzingatia misingi ya katiba na mahitaji ya watanzania. Kwani shida wanazokabiliana nazo hazijui wala kujali dini.