The Chant of Savant

Saturday 13 November 2010

Je waweza kuamini ghorofa 15 kujengwa ndani ya juma moja?


As the United States and China battle over the finer points of currency manipulation at the G-20 summit, American negotiators may want to take note of this startling testimonial to the productivity of Chinese workers: A construction crew in the south-central Chinese city of Changsha has completed a 15-story hotel in just six days. If nothing else, this remarkable achievement will stoke further complaints from American economic pundits that China's economy is far more accomplished in tending to such basics as construction.

6 comments:

Subi Nukta said...

Hawa jamaa wa China wanatuma ujumbe kwa mabepari wa Marekani. Uimara wa nyumba hiyo utaonekana baadaya miaka 10 na ushee kwa maana maghorofa yaliyojengwa na Mjerumani kwetu Ocean Road bado yali imara kama vile yamejengwa tu mwezi uliopita. Tusubiri na tuone hii vita ya tembo itavyoisha, taabu kwetu sisi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Subi usemayo ni kweli. Yetu macho ingawa nasi badala ya kukaa na kuangalia tunahitaji kujisuta kwa kuendelea kuwa kwenye mbeleko ya hawa jamaa.

Subi Nukta said...

Yaani sisi sijui ni mbeleko gani itatubeba Nkwazi kwa maana, hebu fikiria yale magari ya Nyumbu tuliyotengeneza na ile karakana pale Buguruni wamevumbua gari inayotumia mafuta ya taa, kuna mzee mwingine nilimsikia BBC akielezea alivyogundua mashine ya kuzalisha umeme kwa kutumia malighafi rahisi kabisa kupatikana majumbani, lakini nani mwenye dhamana ya uogozi aliyopewa na wananchi anarudisha fadhila ya kuwapigania wavumbuzi wetu hawa waweze kukamilisha uvumbuzi wao? Yaani hata wenye mawazo wanakosa motisha wakiona wengine haawati msaada sana sana wanachekwa tu mitaani. Mwishowe vipaji vinafia mbali watu wanaishi kunywa ulabu na starehe basi, tunasubiri malighafi ngazi ya tatu toka Uchina.

Nashindwa hata kufikiri wakati mwingine kwa nini hali hii.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Subi, usiache kufikiri kutokana na kutawaliwa na mfumo usiofikiri. Tatizo la wezi wetu wanaotutawala ni kuangalia cha juu. Hawataki wavumbuzi wetu waendelee kutokana na kazi zao kuua mianya ya watawala wetu kwenda nje kutuibia kama walivyofanya kwenye rada na dege la rais. Kwao kununua vifaa nje ni dili tupu. Inasikitisha na kukatisha tamaa. Lakini tusiache kufikiri. Maana kuna wakati utafika hata hawa wanaotuibia watabadilika kama tutaamua kuwabana wezi wetu vilivyo.

Subi Nukta said...

Naam, Nkwazi, hawa "watawala" lengo lao ni kuona aidha wengi wanakubaliana na miendendo yao au wanakata tamaa na hivyo kuwapa mianya ya kufanya watakavyo. Nadhani imefika mahali kukaa kimya imetosha, iliyobaki ni kupiga kelele na kuwabana watachoka wataachia ngazi taratibu. Ninawachukia mno "viongozi majina" na "wafu wa fikra wasiopenda kung'atuka", ndiyo hasa kikwazo katika kujendeleza. Eniwei, winners don't quit. Huu ni mwendelezo wa harakati, We will never back down, nor compromise with what is ours. A luta continua, vitoria e certa!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Subi huo ndiyo msimamo muafaka hasa wakati huu tunapotawaliwa na watu wasio na roho, macho wala masikio ukiachia mbali kufikiri kwa matumbo na kuendeshwa na tamaa wao wake zao watoto wao marafiki zao na waramba viatu wao. Tusichoke kuwaghasi hata kuwazomea kama ilivyowahi kutokea kule Mbeya ambapo mawe yaliongea na kuacha aibu ya mwaka ingawa wahusika walijitahidi kuifutika chini ya busati la hekima na taamuli.
Kila la heri,Bis repetita placent.