The Chant of Savant

Wednesday 17 November 2010

Kikwete aendelea kuwalipa fadhila waliofanikisha EPA


-------------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,amefanya uteuzi wa Wabunge watatu(3)kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha,Prof.Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Anne Semamba Makinda(Mb)kwa ajili ya hatua zipasazo.

MWISHO

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010

6 comments:

Msukumamjita said...

Kwa kweli inasikitisha, ni kama vile hao wanasiasa hata wafanye au wasaidie maovu kiasi gani, bado wana uhakika wa kuingia kwenye bunge letu "tukufu", kwa kweli sio tukufu tena, maana utukufu unakuja na kwa uongozi bora, kujali wananchi na kulitumikia taifa kwa hali na mali. Katika viongozi wote hao na watakaokuja, ni "mtoto wa mkulima" peke yake alietangaza mali, wengine hatujaona wala kusoma mali zao!
Sijui tufanye nini sie wananchi tupate haki zetu muhimu za kuendesha maisha yeu?
Nilitegemea wananchi hasa wa vijijini na mjini, wataangalia matatizo yao na kusema basi! Maana hawana maji, wala umeme, elimu ni duni wakati vigogo wanasomesha watoto wao nje, matibabu na kama hakuna, barabara kama ni bahati ni zile zenye vumbi, huduma za ustawi wa jamii ni kama hakuna, rushwa, na utumiaji wa mali za umma ovyo umezidi bila kusahau rushwa iliokithiri!
LINI WATANZANIA MTAJIOKOA???????

malkiory said...

Sikio la kufa halisikii dawa. Huu ni uthibitisho tosha jinsi rais wetu anavyoendekeza ufisadi.

Israel Saria said...

Njia ya kufanya mabadiliko ni kwenye boksi la kupigia kura tu.

Anonymous said...

Unaongelea kura gani na box gani iwapo ni jana tu tumedhulumiwa kwa kuchakachuliwa? Suluhu ni kufanya kweli kwa kuandamana hata kulianzisha aminini.

Anonymous said...

Ujinga huu. Mmemuandama huyu mama na EPA wakati mnajua wazi kwamba EPA hakufanya yeye. Kweli blog ya "mpayukaji"

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nawashukuruni wote mliotoa mawazo yenu ingawa baadhi yenu sikubaliani nanyi. Mchangiaji wa mwisho aliyeficha jina lake bado yuko kizani maskini au ni fisadi mwenyewe au wakala wao. Kuishi kwa kutegemea makobo si stahiki ya binadamu. Tafakari.