The Chant of Savant

Wednesday 17 November 2010

Wananchi wanapouchoka utawala mfu




Picha hii inaacha maswali mengi kuu likiwa, kama tumefikia hapa nani atamtetea na kumlinda mwananchi? Je hawa polisi wanamlinda nani na anawalipa nani? Je hapa mwenye makosa kati ya mwenye rungu dola na bunduki ni nani? Je ni kwanini mwanamme mzima ameamua kuchukua sheria mkononi tena dhidi ya dola lenyewe? Je kwa namna hii bado kuna kondoo wa kuchinja au punda wa kutwisha kila uchafu kama ilivyotokea kwenye uchakachuaji hivi karibuni?
Hivi jamaa huyu wa Uganda angepandikiziwa mbunge kama ilivyotokea Danganyika, huyo mbunge nyemelezi na pandikizi angepona masumbwi ya jamaa huyu? Je wabongo hapa tunapata somo gani hasa wakati huu tunapotawaliwa na serikali fisadi itokanayo na EPA NEC na zoezi zima la uchakachuaji? Je namna hii mlipa kodi ana haja ya kuendelea kuwalipa mishahara watesi wake ili wamtese?
Jibu unalo wewe unayesoma.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Wabongo bado tumefungwa, unyonge umetuzidi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yasinta hujakosea. Tumelishwa limbwata si kawaida. Ila one day yes naamini.

Unknown said...

hadithi ni ile ile ya punda na kipofu!!! wapo wengi wanaoamini kuwa Tanzania tuna maisha mazuri. Ukweli ni kwamba tumelala usingizi mzito na hata hatujui haki zetu ni zipi.