Thursday, 13 January 2011

Kikwete kweli msanii na hovyo


Kama kuna watu wanamuuza na kummaliza rais Jakaya Kikwete, licha ya kukosa busara si wengine bali washauri wake. Hivi, kwa mfano, kwenye picha hiyo hapo juu, alishindwa kutumia common sense kujua kuchagua hata aina ya mavazi? Suti na upandaji miti wapi na wapi? Suti na mbolea wapi na wapi? Kwanini anashindwa kutumia common sense jamani?
Hakika waliosema kuwa Kikwete ni msanii hawajakosea kama mambo ndiyo haya.

Leo utamuona akizindua mradi wa mbolea. Baada ya mwezi kila kitu kimeyeyuka kama tofali la barafu. Je mnakumbuka ilivyovumishwa kwa mbwembwe na hoi hoi kuwa Dar itakuwa na usafiri wa uhakika kwa kuzindua mabasi yaendayo kasi?

Hata huyu upuuzi wa Dowans unaolisumbua taifa, nakumbuka. Rais baada ya kutoka Marekani kuitafuta Richmond, bila kufikiri, alilitangazia taifa kuwa mgao wa umeme utakuwa historia asijue utaweka historia ya kumuumbua.


Baada ya kusoma habari hii na kuangalia picha hiyo hapo juu, hebu soma habari hii hapa chini ulinganishe kazi aliyofanya waziri mkuu wa zamani wa Australia ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje kwa sasa.

2 comments:

Anonymous said...

Yaani mie kaniacha hoi kwa kumwagilia mti maji kwa kutumia glass ya maji ya kunywa! Duh! wakulima wangekuwa hivyo sijui wafanyakazi tungepata wapi chakula!

NN Mhango said...

Huo ndio usanii wanaosema wataalamu wa mambo. Hata hivyo inatoa picha nyingine kuwa mbwa wao huko wanalala kwenye magodoro wakati wakulima wetu wanalalia mbavu za mbwa.
Hao ndiyo watawala wako ndugu yangu. Pole sana.