Wednesday, 19 January 2011

Wafahamu wana wake waliowateka na kutawala marais

Ben Ali na Leila

Kikwete na Salma

Museveni na Janet
Kibaki na Lucy

Mugabe na Grace
Zenawi na Azeb
Mkapa na Anna

Ingawa wengi wanaangalia kwa juu kutimuliwa madarakani kwa rais mwizi wa zamani wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali, ukweli ni kwamba mkewe Leila Trebelsi na ndugu zake 10 ndiyo walimwingiza matatani kutokana na uroho na ujinga wao.

Mama huyu aliyejulikana kama Imelda Marcos wan chi za kiarabu anaamika kutorokana na vito vyenye thamani ya dola za kimarekani 35,000,000.

Msusi huyu wa zamani ndiye analaumiwa kumwingiza majaribuni mumewe kiasi cha kufilisi nchi kutokana himaya ya ukoo wake wa ndugu 10. Ukoo huu ulijiingiza kwenye kila aina ya biashara kuanzia mihadarati, uuzaji magari, internet café, hisa katika mabenki na shirika la ndege la Tunia na mwisho wa yote kama mmoja wa Leila kumilki benki ya Zeitouna ambayo ilichomwa moto sambamba na mahekalu ya ukoo huu fisadi hivi karibuni sambamba na mahekalu ya ukoo huu.

Mwingine katika mchezo huu mchafu ni Grace Marufu Gucchi Mugabe ambaye amepewa jina la Gucchi kutokana na kupenda nguo za fasheni. Ni mama huyu aliyewahi kwenda benki mwaka juzi na kuchukua dola 10,000,000 cash wakati wazimbabwe wakihaha kwa njaa.
Ni mama huyu aliyewahi kumwambia mke mpya wa rais wa Malawi Calista Chapola-Chimbombo kuwa kama mke wa rais atumie na kufanya atakacho bila kusikia wambea (wananchi) wanasema nini. Ni mama huyu huyu ambaye amemnunulia bintie Bona Mugabe hekalu huko Hong Kong anakosoma. Binti hiyi mchanga ana watumishi huko Hong Kong karibu idadi sawa na wafanyakazi wa ubalozi wa Zimbabwe kule.

Watu wengi hawamjui mke wa waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi aitwaye Azeb Mesfin au Queen of Mega (Corruption) kutokana na kujihusisha na ufisadi wa kiasi cha kuu au mega corruption kwa kimombo. Huyu kama Leila ana himaya ya biashara nchini Ethiopia na nje si kawaida.

Bila shaka wote mnamjua Janet Keinembabazi Kataha Museveni mke wa dikteta wa pili wa Uganda Yoweri Museveni. Huyu amehakikisha ukoo wake, wakwe zake, wajomba zake, dada zake na kila anayemhusu kuwa marais wadogo nchini Uganda. Kimsingi, ndiye mshauri mkuu wa Museveni ambaye kwa pamoja licha ya kuunda utawala wa kabila lao la wanyankole, wameunda urais wa familia. Nani alitegemea angeteuliwa na mumewe kuwa waziri baada ya kuonyesha tamaa ya siasa? Wapo wanaodhani anaotea kumrithi mumewa kama alivyofanya rais wa sasa wa Argentina Cristina Fernandez Kirchner.

Naye Salma Kikwete na Rahma al-Kharoos bi. mdogo wa Kikwete nao hawajaachwa nyuma tokana na kuwa na mashirika na biashara zao zilizotundikwa nyuma ya mgongo wa ikulu. Salma ni rais wa WAMA. Na Rahma ni rais wa kampuni ya mafuta ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED.

Salma alirithi uroho na upogo huu toka kwa Anna Mkapa ambaye aliutumia utawala wa mumewe kufanya kama Leila yaani kuneemesha ndugu na marafiki zake. Rejea kashfa ya Net Group ambapo mmojawapo wa wakurugenzi wa kampuni iliyoleta kampuni hii toka Afrika kusini kuwa mtoto wa darasa la tano wa kaka yake Anna.
Lucy Kibaki naye si haba. Kufumka kwa kashfa ya mahindi nchini Kenya kulimuacha uchi baada ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa biashara zake.
Je wananchi wanapanga kuwafanya nini watawala wanaotawaliwa na wake na vimada wao?

9 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Hii "COLLECTION" sikuwahi kuiona.
Nimeisoma na naitafakari

NN Mhango said...

That is it. Ni Changamoto hasa kwa wazee wa changamoto kama wewe.Mbona wapo wengi ila tumetoa wale waliokubuhu kwa uchafu na udhaifu wa kutawaliwa kiasi cha kusahau viapo vyao.

Mzee wa Changamoto said...

Basi wacha nilifanyie kazi hili. Ninafurahi ninapotembelea VITUO VYENU WAUNGWANA ninapata changamoto zaidi za kusaka mengine zaidi ili kuwapasha wananchi mengi zaidi
BLESSINGS

NN Mhango said...

Sisi sasa ni familia ya ukoo wa Thinkers.
Karibu sana TENA NA TENA hata mie huwa napitia kwako mara nipatapo muda kutokana na kubanwa.

Yasinta Ngonyani said...

Ni mkusanyo mzuri ambao wengi hawaujui umefanya vizuri kakangu kwani ni viruri kujua nimefurahi kwani nilikuwa sijui huu ndio upekuzi tuotakao.

NN Mhango said...

Asante Da Yacinta kunitembelea. Ni kweli. Tunahitaji kubukua kweli kweli ili kuwawezesha watu wetu wasome ingawa hawana mila hiyo zaidi ya kukimbilia picha na kukwepa kusoma na kuumiza vichwa. Kwa atakayekubali kujisulubu na kusoma maisha yake yatakuwa mazuri hata awe chini namna gani.

Yasinta Ngonyani said...

Kakati jamii yetu ya Tanzania kusoma sijui ni mwiko maana mtu anakubali kwenda kilabuni kuliko kusoma kwa kweli inasikitisha san. Inahitaji UHAMASISHAJI MKUBWA SANA.

Anonymous said...

Yasinta, mwamko ni mkubwa sana, imefika mahali ukisafiri kwenda kijijini watu wanakuuliza gazeti liko wapi badala ya mkate kama zamani tulivyozoea!

Kwa taarifa yako shida na ugumu wa maisha vimetufanya tunasoma kila kila kitu so long as kina maandishi.

Sirili

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi kama hawaulizi kuhusu mkate na wanauliza kuhusu gazeti safi sana. Ahjsante kwa taarifa kwani inaletesha furaha