The Chant of Savant

Friday 21 January 2011

Kizazi kipya cha ndege chatangazwa


Lockheed imekuja na hii

Northrop Grumman imetoka na kitu hiki

Nao Boeing hiki ndicho kifaa chao



Shirika la Mambo ya Anga la Marekani (NASA) limetoa mifano ya ndege zitakazotumika kufikia mwaka 2025.

Shirika hili lilitoa tena kwa makampuni ya Lockheed Martin, Northrop Grumman na Boeing mwishoni mwa 2010 kutengeneza ndege yenye kwenda kwa angalau 85% ya mwendo wa sauti. Pia ndege hii ilipaswa kutochafua mazingira, yenye kutumia mafuta kidogo na isiyopiga kelele na iwe tayari mwaka 2025.

Kadhalika, ndege hukika ilipaswa kuwa na uwezo wa kubeba mzigo kuanzia kilo 22,680 hadi 45,360.

Aina tatu za disaini ya ndege hii ya kimapinduzi imewasilishwa na makampuni husika kama unavyoona kwenye picha. kwa wale mashabiki wa ndege kama mimi hii ni habari kubwa tu.The three designs submitted by the companies are radically different.

Disaini inayoonyesha kuvutia ni ile ya Martin Lockheed yenye injini ya ndege iliyoningèinizwa mkiani mwa ndege.
Wengi wanahofia kama ndege hii itaanza kutumika kama ilivyolengwa kutokana na Boeing Dreamliner 787 iliyoanza kutengenezwa mwanzoni mwa 1990. Hata hivyo imekumbwa na mikwamo kibao kiasi cha hata sasa miaka kumi baadaye kuwa bado haijazoeleka ikilinganishwa hata na Airbus 380 dege lenye uwezo wa kubeba watu kibao kuliko nyingine duniani.

Kutokana na tatizo hili la Dreamliner ndiyo maana NASA ikaanza kufikiria ndege ya 2025 mwaka 2011.
Mambo ya teknolojia hayo.
Chanzo: Internet.

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kwa sisi tunaotengeneza vifaa (parts) na vipuri (spare parts), ndio maana twaanza kuona ongezeko la kazi kwa mbaaaaaaaali.
Na wazilete tuuuuuu
Ilmradi ni salama kwa abiria

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nadhani usalama wa abiria na mazingira vimezingatiwa sana bila kusahau kuokoa muda. Je Bongo madude haya yatafika lini? Hii ni changamoto kwetu.