Friday, 28 January 2011

Je hawa jamaa unawafananishaje?


Kwangu wote wana majina yanayoanza na herufi J. Pia hakuna mtaji uliowaingiza madarakani zaidi ya umaarufu na kuwavurugia wenzao. Jakaya Kikwete aliwatumia waandishi wa habari nyemelezi wakiongozwa na Salva Rweyemamu kuwachafua akina Fredrick Sumaye Salim Ahmed Salim na wengine waliokuwa tishio.

Jacob Zuma alimsukia zengwe rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na kuchukua nafasi yake.

Wanapenda matanuzi na kuruka ruka nje ya mchi. Wanapenda kuvalia suti za bei mbaya.
Wana watoto wengi hata wengine hudiriki kusema nyumba ndogo.Pia wana kasheshe za mambo ya down. Rejea kufungwa kwa mwanamuziki mmoja wa DRC aliyekuwa akifanya shughuli zake za muziki Bongo.Zuma anasifika kwa kubaka sawa na Kikwete ambaye amebaka demokrasia nchini Tanzania kwa uchakachuaji.

Kiakili wote wako sawa ingawa mmoja ana shahada na mwingine hana hata darasa moja.

Wote wanaongoza nchi zenye raslimali nyingi. Tofauti na Kikwete, angalau kwa Zuma raslimali zile zinalinufaisha taifa hasa wazungu.

Wote wameruhusu watoto wao kuwa rais wadogo. Hapa tunaongelea Ridhiwani na Duduzane almaarufu Dudu ambao wanatumiwa na wafanyabiashara na wasaka ngawira kuyaibia mataifa yao.

Hawa jamaa wanawaweza kuwa mapacha. Kazi kwako kuongeza sifa nyingine zinazofanana walizo nazo.

1 comment:

Anonymous said...

WOTE HAWA NI WAZINZI NA WEZI HAWAFAI NA WANAFANANA KWELI KWELI.
MCHANGANUO MZURI SANA. WATUMIE KOPI OFISI ZAO KAMA INAWEZEKANA.