Friday, 25 February 2011

Angalia wenye utu na akili na si mafisi wetu

WASOMAJI WANGU WANANISIKITISHA KUTOACHA UJUMBE LAU NUSU MSTARI.

Marie na Ollier pichani

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Michelle Alliot Marie ameamua kujiuzulu baada ya kugunduliwa kuwa yeye na mchumba wake Patrick Ollier walikodishiwa ndege na mshirika wa rais wa zamani wa Tunisia, Zine al Abidine ben Ali.

Wawili hawa ambao wote ni mawaziri Ollier akiwa waziri wa masuala ya uhusiano wa bunge walitenda kosa chini ya sheria za Ufaransa.

Marie angekuwa waziri wa ulinzi wa Tanzania ambapo mabomu yameua makumi ya watu wasio na hatia huenda angejinyonga ili kutubu dhambi yake.

Marie alipotakiwa kujiuzulu hakutafuta visingizio wala kuzungusha bali kukiri na kujiuzulu huku akiomba msamaha. Hili ni suto kwa mawaziri wetu kama Dk. Hussein Mwinyi ambaye kung’ang’ania kwake madaraka kumemuondolea heshima aliyokuwa akipata kutokana na kazi nzuri ya baba yake.

Wapo waliowahi kusema kuwa alikuwa akiandaliwa kuwa rais wa Zanzibar. Lakini kwa doa alilopata hili haliwezekani tena.

Mwinyi angesoma habari za wenzake ili ajifunze lau kujisuta na kujiwajibisha badala ya kungoja kusukumwa kama akina Mubarak na Gadaffi.
Bahati yake, Jakaya Kikwete, bosi wake naye amechafuka kiasi cha kukosa busara na ithibati ya kumwajibisha kwa vile roho yake inamsuta.

2 comments:

MwaJ said...

Kwa kweli inashangaza alivyo na roho ngumu na hata kukosa aibu!Sijui kwa nini viongozi wetu wanaogopa sana hili suala la uwajibikaji! Ndio sababu hata wale walio chini yao hawajali kitu na kubaki kucheka cheka tu na kujibu kwa mzaha kuwa "milipoko ya mbagala haikujirudia maana milipuko ya sasa ni ya gongo la mboto! Pyuuuuu!

NN Mhango said...

Mwa J,
Usemayo ni kweli. Walioko chini wanapewa kiburi na wakubwa wao maana jogoo aliwafundisha vifaranga kunya ndani.
Shukrani kunitembelea na karibu tena.