Friday, 18 February 2011

Mauaji ya Gongo la Mboto Dk Mwinyi anangoja nini kujiuzulu?Kwa wanaokumbuka mauaji ya kizembe yaliyotokea na milipuko ya mabomu kwenye maghala ya kijeshi kule Mbagala mtakumbuka viapo na ahadi vya serikali hasa waziri mhusika Dk Hussein Mwinyi.

Aliahidi kuwa maafa haya yasingetokea tena. Alitoa ahadi hii wakati akipinga shinikizo la kumtaka ajiuzulu ikiwa ni kama kuomba fursa kutokana na lile kuwa kosa la kwanza. Sasa kabla hata waliofariki Mbagala kuoza, Dk Mwinyi ameanikwa. Je anangoja nini kutekeleza ahadi aliyoitoa kwa hiari yake?

tunajua aliyepaswa kuwajibishwa ni serikali nzima. Ila kwa utawala mfu na mbovu tulio nao hili sahau.

Kwanini Dk Mwinyi haigi mfano mwema wa baba yake aliyejiuzulu kutokana na vifo vya watu wasiofikia hata kumi ikilinginshwa na halaiki iliyouliwa na mabomu kutokana na uzembe wa wizara yake naye binafsi akiwa mkuu wa wizara. Je maafa ya Mbagala na Gongo la Mboto si ushahidi kuwa utawala wetu ni wa kizembe na usiojali maisha ya watu wake?

Hebu soma nukuu ya rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiongolea mkasa huu.
Alikaririwa akisema: "“Haya ni maafa ya kitaifa, kwa sababu kikosi hiki ndio makao makuu ya hifadhi ya kijeshi, ikiwemo silaha na mavazi yao ambayo mpaka sasa hivi naongea vyote vimetekelea kwa moto.”

Aliendelea kuonyesha ubovu wake kwa kusema, "Kwa taarifa nilizonazo ni askari mmoja aliyejeruhiwa, hivyo basi ninawaomba wananchi waondoe wasiwasi juu ya tukio hilo, Serikali iko pamoja nao kuhakikisha kuwa hatari zilizopo zinadhibitiwa, na kwamba wananchi wanarudi katika hali yao ya kawaida.”
Kwa ufupi ni kwamba tuna watawala wasio na roho bali uroho. Hawana huruma wala utu bali makatili na fisadi wa kupita kiasi.

4 comments:

Jaribu said...

Hata mimi nilishangaa kauli hiyo. Mwanajeshi mmoja amekufa? Wanajeshi ndio waliosababisha ajali hiyo. Hao wengine raia hawastahili kutajwa au kujaliwa. Shida ni kwamba haa viongozi aibu au maybe hata conscience, hawana.

NN Mhango said...

Jaribu usemacho ni kweli. Tuna viunguzi si viongozi. Hata kuwaita watawala ni kuwapendelea. They are but criminals that are accidentally in power they are misusing and abusing.

Anonymous said...

Hawajui watendalo wanaona kuwa wananchi hawana maana yoyote kwao. Wanatoa idadi ya uongo ya wananchi waliopoteza maisha yao. Hii serikali ni ya vilaza watupu wasiojua chochote. Wanachojua ni kuiba pesa Za wanachi. Kujieleza ni zero; siku zote ni kuongea pumba.

Mwaj said...

Katika yote inasikitisha sana maana bado kuna wazazi hawajawapata watoto wao. Hebu fikiria mtu hujui mtoto wako alipokimbilia hujui kama yuko hai au la! Ni uchungu na mashaka kiasi gani? Kisha mtu anakuja na kauli kuwa serikali itagharamia mazishi! Unajitapa kugharamia mazishi kwani ndugu zetu wamekufa vifo vya kawaida? Nani anataka kusaidiwa kuzika hapa tunachotaka ni uzima na usalama wetu wakati wote na sio kusaidia kutuzika! Yaani mijitu inatia hasira sana!