Friday, 11 February 2011

Hatimaye umma waangusha gogo liitwalo Mubarak
Imetangazwa rasmi kuwa imla wa Misri Hosni Mohammed Mubarak amebwaga manyanga baada ya shinikizo la umma kushinda. Ni furaha si kwa wamisri tu bali dunia nzima hasa Afrika ambako kuna Mubarak wengi tu.

Japo inatia shaka busara iliyotumika kulikabidhi jeshi madaraka, kuna haja ya kutopoteza matumaini kutokana na jeshi lilivyochangia kumwangusha Mubarak baada ya kugoma kumuunga mkono.

Hili ni somo tosha kwa majeshi mengine ambayo yamegeuzwa nepi za watawala wezi.
Je kuanguka kwa Mubarak ni mwanzo wa mwisho wa uimla barani au kizazi kipya cha vuguvugu la ukombozi wa pili na wa kweli wa bara hili?
Je baada ya Mubarak nani atafuatia? Libya, Algeria, Sudan, Morocco, Mauritania, Saudia, Yemen, Jordan, Kuwait na Afrika Kusini mwa sahara kuondoa Afrika Kusini, Botswana na kidogo Kenya watawala wamo msambweni. Je nchi yangu ya Tanzania itanusurika? Je ushindi huu ni wa umma au wanajeshi? Nini kitafuatia? Ni swali gumu kujibu.

No comments: