How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 29 August 2012

Mchungaji au mchunaji, injili au unga?







    Hapo juu ni hekalu jipya la anayejiita mchungaji Getrude Rwakatare lillilozinduliwa huko Mbezi Beach  nje kidogo ya jiji la Dar es salaam hivi karibuni. Wengi wanajiuliza. Huyu ni mchungaji au mchunaji? Je huu utajiri wa ghafla ameuchuma wapi na kwa muda gani na kwa kufanya nini? Kweli Tanzania imegeuka nchi ya wanyang'anyi ambapo mtu anaweza kulala maskini akaamka tajiri na hakuna anayeuliza. Je Rwakatare anafanya biashara gani na analipa kodi kiasi gani? Tuna haja ya kuuliza hasa baada ya kugundulika kuwa Rwakatare ni mmojawapo wa watu waliokamatwa wakitumia umeme wa wizi. Jumba kama hili ukilijenga kama hapa Kanada ujue utatozwa kodi hadi ukome. Isitoshe huwezi kuwa na utajiri ambao hauna maelezo kabla ya mamlaka ya kodi kuuweka mikononi hadi utoe maelezo yanayoeleweka ulivyochuma. 

6 comments:

Mbele said...

Yesu aliishi maisha ya mtu wa kawaida sana. Tena alisema kuwa mtu huwezi kumtumikia Mungu na pia mali.

Yasinta Ngonyani said...

Kila kitu siku hizi ni biashara tu..huo si uchungaji bali ni uchunaji..yaaani hasi makanisani..

Anonymous said...

Kama hekalu la Rwakatare ni hivi hilo la Ridhiwan au Chenge yakoje? Nchi yetu inakwenda pabaya. Hekalu kama hili haliwezi kutokana na sadaka huenda kuna biashara nyingine bila shaka unga au hata ujambazi kama siyo kutumia kanisa kupata misamaha ya kodi na kupitisha biashara za wafanya biashara.

Anonymous said...

Na nyie gombeeni ubunge mpate misamaha ya kodi. Ila Lwakatare alianza siku nyingi kutafuta pesa na kutoa huduma hasa za elimu kupitia shule za Saint Marry`s. Kwahiyo na nyie tafuteni pesa wapenzi. SI lazima ujenge jumba unaweza kufanya mambo mengine. Ila kodi ya mali (property right inatakiwa kuwa ya kutosha labda millioni ishirini hivi. Hapo hiyo nyumba itakuwa imetusaidia kama walala hoi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka Mbele, Dada Yacinta kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Kaka Mbele nilipita kwako siku moja nikakuta kumbe nilichelewa kukutakia siku njema ya kuzaliwa. Dada Yacinta usemayo ni kweli usishangae kukawa na miunga na uchafu mwingine nyuma. Anon wa kwanza nakubaliana nawe ingawa huyu wa mwisho ameonyesha kushabikia wizi huu. Huwezi kusema eti kodi atakayolipia nyumba itasaidia walalahoi wakati Tanzania watu hawalipi kodi. Muhimu ni kuhoji alivyochuma huu utajiri. Shule za St. Mary ni matokeo ya utajiri uliofichika. Tuzidi kudodosa alipopata pesa huyu mama na wengine kama yeye. Tunaweza kushabikia ufahari wao wakati ni mauti yetu iwapo watabainika kutolipa kodi au kutumia makanisa yao kupitisha biashara za watu na kulipwa wao ukiachia mbali biashara ya mihadarati.
Nawakaribisheni tena kwenye kisebule changu.

Anonymous said...

Kweli huyu msimbe na nungaembe ni mwizi na fisadi wa kawaida.Huwezi kujenga hekalu kama hili bila kuiba kwa nchi kama yetu iliyokuwa ya kijamaa jana tu. Ulaaniwe Rwakatare na ulegee. Ni kweli pia anaweza kuwa muuza unga huyu anayejificha kwenye uchungaji.