How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 10 August 2012

Tanzania kuna mfumo-kristo au mfumo-islam au bangi za wanaodhani hivyo?



Nikiwa napita pita kwenye wavuti wa Jamii Forums jana nilikutana na hoja kuwa 'mfumo-kristo umeleta umaskini nchini Tanzania. Hoja hii ilinivutia na kunichochea kuandika yafuatayo kama majibu kwa wale wanaoota mchana na kutafuta visingizio badala ya kukabiliana na tatizo lenyewe.
Niliandika:
Huo uislam na ukristo zaidi ya kuleta utumwa na ukale umeleta nini? Tatizo la Tanzania si mfumo kristo wala dini bali utawala mbovu. Ukiangalia ufisadi uliofanyika chini ya utawala wa Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi na sasa Jakaya Kikwete, unashangaa maana ya mfumo-kristo kama kweli upo nayo ipo.
Ukiangalia watuhumiwa wakuu wa ufisadi kama vile Andrew Chenge, Edward Lowassa Idd Simba na Idris Rashid wote ni wa dini zote. Tutafute jawabu sahihi la tatizo letu badala ya kutafuta visingizio. Inashangaza mtu mwenye akili timamu kusema eti Tanzania inaongozwa kwa mfumo kristo wakati rais na makamu wake ni waislam. Mtu wa namna hii ima hajasoma na kuelimika au ni kasuku anayejipayukia bila kufikiri wala kufanya utafiti. Huu upuuuzi "wa mfumo kristo" sasa umegeuka kuwa wimbo kwa watu wasiokuwa tayari kufikiri sawa sawa. Nendeni vijijini muone watanzania wanavyoumia bila kuangalia dini wala watokako. Kuna haja ya kuacha uvivu wa kufikiri na kutafuta visingizio. Tatizo la Tanzania ni utawala mbovu wa kifisadi unaoendekeza kuombaomba na kutumia vibaya. Nyerere aliwahi kusema kuwa uchumi mnao lakini mmeukalia. Wajinga walitafsiri kipuuzi na kukosa maana na nafasi ya kukabiliana na changamoto ya umaskini. Hakuna cha mfumo kristo wala islam.

2 comments:

Anonymous said...

napenda kutoa maoni kwa wanaosema kuwa mfumo kristo ndiyo umeleta umasikini.nami nasema kuwa baadhi ya watanzania wanasubiri kutafuniwa tu na kuiba yaani wizi. Mungu anasema katika kitabu cha mwanzo,utakula kwa jasho lako je nakuuliza wewe mlalamishi umetafuta ukakosa au ni lalama tu, pia ukumbuke hukuumbwa na serikali umeumbwa na Mungu na mungu anakuwazia yaliyo mazuri , soma kitabu cha mathayo kinasema tafuteni nanyi mtapata ombeni nanyi mtapewa, sasa kama ukiitegemea serikali utakufa masikini.hakuna cha mfumo kristo wala islam ni kuosa maarifa tu. elekeza jicho kwa Mungu tuache kuangamia kwa kukosa maarifa hayo, tujifunze kwa Mungu tusiwe tegemezi kwa serikali,serikali siyo iliyokuleta duniani poleni sana kwa kuitegemea .Rebby

Anonymous said...

Anon hapo juu ni mpuuzi wa wapuuzi.