How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 3 August 2012
Ufaransa yaanza kukamata mali za mafisadi wa kiafrika
Hilo hapo juu ni hekalu la ghorofa sita mali ya mtoto wa rais wa Equatorial Guinea, Teodorin Obiang Mangue (43) ambaye pia ni makamu wa rais wa baba yake iliyokamatwa na serikali ya Ufaransa nchini humo hivi karibuni. Jumba hilo lina thamani ya kati ya Euro 100,000,000 na 150,000,000. Na hii siyo mali pekee ya mtoto wa rais Theodoro Nguema Obiang Mbasogo bali sehemu ndogo ya mali zake zilizotamalaki dunia nzima. Ana majumba Amerika, Ulaya na kwenye visiwa mbali mbali vya maraha. Je ni watoto wangapi wa watawala wezi wa kiafrika watafuatia hata kufikishwa mbele ya vyombo vya kimataifa vya sheria? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Wao wenyewe mijizi sasa wanamkamata nani hilo changa mtapigwa nalo nyie sie tunaendelea kutamba aaa hakuna kukamatwa wala kufumaniwa mali ya kiongozi gani wa ki aaaaaaafrika imekamatwa mpaka leo usilete uwoza hapa.
mabutu seseko kuku wa zabanga mali uloiba iko wapi
Post a Comment