“Vitendo vya
kuchambuana mwishowe ili mharibiane mwishowe mnakuwa dhaifu.. vita ya panzi
sherehe ya kunguru,” Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa chama chake .
Alitoa maneno haya wakati akikemea wanaoutafuta urais baada yake. Kwa
wanaofahamu jinsi Kikwete alivyoasisi mchezo wa kuchafuana akiwatumia hired
guns kama Salva Rweyemamu na waandishi wengine wa habari nyemelezi na wachumia
tumbo, wanashangaa Kikwete anapata wapi jeuri ya kuwananga wenzake. Je ni yale
yale ya nyani haoni kundule au unafiki wa
kawaida? Je Kikwete ana udhu wa kuwananga wenzake wakati yeye ndiye mwanzilishi
na mnufaika wa jinai na kadhia hii?
Hebu angalia
nukuu nyingine ya Kikwete, “Niacheni…. nitakuwa mwenyekiti wa ajabu sana, eti
wanataka niwe kwenye kambi zao hivi nikiwa kwenye kambi zao nitatenda haki?”
Kweli Kikwete
haishi maajabu na sanaa. Haki gani anaweza kutenda iwapo ameshindwa kutenda
haki ya kutimiza ahadi zake? haki gani anayoijua Kikwete iwapo utawala wake
umeghubikwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu? ni haki gani anayoongelea
Kikwete iwapo ameshindwa kutenda haki ndogo tu ya kukemea mafisadi achilia
mbali kuwakamata?
Kikwete ataondoka madarakani na kuacha historia ya kuwa rais asiyeeleweka wala kuelewa. Ataacha legacy ya kukuza na kudumisha ufisadi na ugeugeu hata mahali pasipostahiki.
Je maneno ya Kikwete ni ya kuamini na kuaminika iwapo anajulikana yupo kwenye mtandao upi? Je kwanini Kikwete anadanganya na kujidanganya mwenyewe? Hakika time will tell.
No comments:
Post a Comment