The Chant of Savant

Monday 12 November 2012

Kenya yapoteza polisi 42!

Injured police officer in hospital
Ingawa sakata la wizi wa mfigo nchini Kenya linaonekana kama la kawaida, mwaka huu limechukua sura mpya baada ya wezi wa mifugo kuvamia askari na kuua 42 na kujeruhi wengine wengi. Sakata hili lilitokea kwenye eneo la Samburu ambapo wafugaji humilki bunduki ili kujihami dhidi ya wavamizi toka nchi jirani. Serikali imepata somo kwa njia ngumu baada ya kupoteza idadi kubwa namna hii. Je huku kuzagaa kwa silaha si kitisho kwenye eneo zima? Je dawa ni nini zaidi ya kuhakikisha kuwa Somalia inakuwa na serikali imara? Kuna haja ya kuliangalia janga hili kwa macho mapana. Majirani wanapaswa kuanza kujiandaa kupambana na madhara yatokanayo na kuzagaa kwa silaha. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: