Thursday, 7 February 2013

Marais vihiyo na malimbukeni ni hatari kwa uchumi Afrika


Taarifa kuwa rais Joyce Mtila Banda wa Malawi analenga kutumia mamilioni ya Kwacha kubadili picha yake ili kuendana na shahada ya PhD ya dezo aliyozawadiwa hivi karibuni ni machukizo kwa walipa kodi. Banda rais aliyeingia madarakani baada ya kifo cha Bingu wa Mutharika ameonyesha sura yake halisi kuwa ni mpenda sifa na asiyejali maslahi ya wananchi. Ni bahati mbaya kuwa na rais limbukeni na kihiyo aliyeta tayari kupoteza pesa ya umma ili kufaidi sifa asiyo kuwa nayo. Hakuna kitu nachukia kama shahada za kupewa zinazowalewesha watawala wetu kiasi cha kuua elimu kwa vile wana njia ya kupata shahada. Ni bahati mbaya jinai hii sasa inaanza kuhalalishwa hadi kufikia mawaziri kughushi shahada bila kuchukuliwa hatua. Nadhani Tanzania inaongoza kwa jinai hii ambapo kuna mawaziri waliotuhumiwa wazi kughushi lakini hawakuchukuliwa hatua. Nani atawachukulia hatua wakati bosi wao yaani rais naye ni mpenzi na shabiki wa shahada za sokoni? Kwa habari zaidi GONGA HAPA.

2 comments:

Jaribu said...

Hata Bingu wa Mutharika naye alikuwa na Phd ya kununua. Viongozi wetu wanakatisha tamaa.

NN Mhango said...

Hata mimi sikujua. Nilitokea kumheshimu na kumuona msomi. Baada ya kujua nimemdharau sana hata kama ameishakufa. Hatuna viongozi bali mafisi na mbwa mwitu ambao wako tayari kuuza roho na miili yetu kutaka sifa na utukufu. All this is because of ignorance.