Monday, 25 February 2013

Vunja mbavu ya leo: Rais Salma ahenyesha wakuu wa mkoa wa Rukwa

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisoma taarifa juu ya sekta ya afya mkoani kwake kwa Salma Kikwete mke wa Rais ambaye naye anapokelewa kama rais kila aendapo.Salma akizidi kuwahenyesha watendaji wa mkoa wa Rukwa. Huyo hapo juu ni  mganga mkuu wa Hospitali ya Rukwa Gurisha Richard naye akichukua zamu yake kujikomba kwa mama rais. (Picha zote kwa hisani ya Jamii Forums)

14 comments:

Anonymous said...

HUU SASA UFALA mkuu wa mkoa unapiga magoti kwa salma yeye ni nani acheni umbumbumbu,na kuto jiamini kwani ukiacha ukkuu wa mkoa hautaishi? mumeniuzi sana

Anonymous said...

Heri ufala kuliko ufarasi na upunda. Injinia mzima anampigia magoti kihiyo kama Salma. Kweli njaa ya kichwani ni mbaya kuliko ya tumboni.

Anonymous said...

Hii inatisha. Yaani hawatendaji ni kweli hawafahamu "ILANI" ya ajira zao kuwa wanawajibika kwa nani? Sasa Salma asiporidhishwa na ripoti, je ana nguvu ya kuwafuta kazi? Au ni kutojiamini kwao tu ndiyo wamekubali kudhalilishwa hivyo? Au ni kulipa fadhila ya aina fulani?

Hivi Salma si mwalimu wa "Grade A"? Si nia yangu kudhalilisha walimu, kamwe! Lakini anapata wapi "nguvu" hii?

Tuamke waBongo!!!!

Anonymous said...

Lakini msimwonee Salma kwani wanaƶtakiwa kufanya kazi hizi hawafanyi ili mradi wamuangushe Rais kwa mtazamo wangu ameamua kumsaidia mumewe kwani tatizo ni nini jamani? kama anachokifanya ni kwa maendeleo ya jamii hakuna shida

Jaribu said...

Anonymous wa 26 February 2013 09:11

Hamna mtu anayemuangusha Rais anajiangusha mwenyewe. Kama hao hawawezi kazi, Rais awafukuze; siyo kumtuma mkewe. Shida ni kwamba hawezi kuwawajibisha wateule wake wasije wakatoboa siri. Ni kama vile mtoto mdogo anayefijicha nyuma ya kanga ya mama yake!

Anonymous said...

Kikwete anajiangusha ili iweje? Unataka kusema Salma yupo juu ya Kikwete siyo? Waswahili kwa kufyatua maneno! Mie napita tu.

Anonymous said...

HHaloo wacheni kutapika matapishi ya ulevi wa kienyeji hata wewe wacha kupiga magoti ungeligaragara mbele ya mama salima heshima mbele kwa mke wa rais wakuu.
mwanamke wa kwanza TANZANIA.
hata kipofu anaona.watu wana macho ya kubandika
HESHIMA KWA MAMA sALMA KWA KAZI ANAYOIFANYA

Jaribu said...

Anonymous wa 26 February 2013 14:49

Sasa na huyo aliyesema watu wanamwangusha Rais anamaanisha nini, wanampiga ngwala?

Jaribu said...

"HESHIMA KWA MAMA sALMA KWA KAZI ANAYOIFANYA"

Kazi gani hiyo? Nyie ndio Wazungu wanawaita "Walamba makalio!"

Anonymous said...

WATANZANIA LAZIMA TUBADILIKE MKE WA RAIS ANA MCHANGO MKUBWA KATIKA JAMII
TUNAISHI DUNIA YA UTANDAWAZI WENZETU PIA WAKE AU WAUME WA MARAISI WANA MAJUKUMU KATIKA JAMII, KWA SABABU WANAISHI KARIBU KULIKO MTU YOYOTE KWA RAIS NA WANAJUA MENGI KULIKO MTU YOYOTE NA NDIYO WAFARIJI WAKUBWA WA MARAIS ,SIONI SABABU KULALAMIKA KAMA WANAFANYA KAZI ZA JAMII TUSIWE NA WIVU WA KIPUMBAVU HASA WANAPOFANYA KAZI ZA JAMII

Anonymous said...

Anonymous hapo juu umetoa utumbo mtupu. Kuwa karibu na rais isiwe kibali cha kuibia umma. Salma ni mwizi kama mwizi yeyote.

Anonymous said...

Hvi huyo Mama kazi zake ni zipi, kumwakilisha raisi mikoani asipo kuwapo? Hizo taarifa ni za nini? yeye zitamsaidia nini? KUombea misaada zaidi? Akisha pata hiyo taarifa halafu hajaridhishwa nayo anaiwakilisha wapi? kwenye baraza la mawaziri au ikulu?

Anonymous said...

Bado sipati picha walikuwa wanamweleza kitu gani?!

Anonymous said...

Huyo shosti anaganga njaa kama Anna Mkapa. Urais umegeuzwa wizi kwa umma ambapo wake na watoto wa rais huiba kwa kutumia kofia ya urais. Ni aibu kuwa na wezi wanaojificha nyuma ya mgongo wa bwana mkubwa. Haya hakika ni matumizi mabaya ya madaraka watanzania tuamke kama alivyosema anonymous hapo juu.