Ingawa serikali ya Tanzania na rais Jakaya Kikwete wameziba masikio kuwatimua mawaziri wanaotuhumiwa kughushi shahada zao, nchi nyingine hazina mchezo na jinai hii. Hivi karibuni nchini Ujerumani waziri wa
Elimu, Annette Schavan alilazimika kujiuzulu si kwa kughushi shahada bali kuiba baadhi ya maandiko kwenye tasnifu ya shahada yake ya juu ya PhD ambayo chuo kilichoitoa kimeibatilisha. Ni hivi karibuni dunia ilijua kuwa kumbe rais wa zamani wa Malawi Marehemu Bingu wa Mutharika alikuwa na PhD feki. Hii ilibainika baada ya rais wa sasa Joyce Mtila Banda kutaka kutumia mamilioni ya Kwacha kuchapisha picha zake upya ili kuonyesha kuwa ni 'daktari' baada ya kugawiwa shahada hiyo na chuo kimoja nchini Korea. Hii si mara ya kwanza kwa Ujerumani kumfurusha waziri kwa kunukuu maandiko ya wengine bila kutaja. Waziri wa zamani wa Ulinzi, Karl-Theodore Zu Guttenberg alitimliwa kwa kosa hilo hilo. Ni ajabu kwa Tanzania mawaziri kama Mary Nagu, Emanuel Nchimbi, Makongoro Mahanga na baadhi ya wabunge na mabalozi wanaendelea kututia aibu katika ofisi za umma. Kwa habari zaidi GONGA HAPA.
No comments:
Post a Comment