Friday, 22 February 2013

Salma anapoufukuzia ubunge!

Siku hizi hatambulishwi kama mke wa rais bali mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Kwa wenye akili, uzoefu unaonyesha kuwa mama amenogewa ulaji na sasa anautaka ubunge hasa baada ya mumewe kung'atuka. Kuna uwezekano wenzetu hawa kila mmoja ana lake. Anna Mkapa alimtumia Mkapa kujirundikia mali huku Salma akimtumia kwa yote mawili yaani kujirundikia mali na kutafuta ulaji wa kisiasa kwenye chama cha mumewe. Kwa wanaojua uwezo wake, wanashangaa muda anaopoteza kwenye kusaka utajiri na madaraka badala ya elimu. Je hii inatoa picha gani kwa taifa letu? Hakika hii nayo ni aina fulani ya matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi.

No comments: