Sunday, 6 October 2013

Mjue FIsadi wa IPTL James Rugemalira


Kwa waliofuatia kashfa na hujuma ya kampuni  ya kuzalisha umeme ya IPTL watakuwa wanakumbuka jina James Rugemalira tapeli na fisadi aliyewezesha wahindi wenye kampuni hili la Malaysia kuiingiza Tanzania kwenye moja ya hujuma kubwa na chafu za kiuchumi duniani. Nilishangaa kumuona akiwa ameibukia kwenye biashara ya bia ambapo ameweza kutumia chumo lake la wizi kuanzisha kampuni ya bia ya Mabibo. Amejipa cheo cha mshauri wa biashara wa kimataifa wa kampuni hiyo wakati ukurugenzi akimpa binti yake aitwaye Benedictor. Ni bahati mbaya kuwa watanzania ni kondoo ambao hawawezi hata kuamua kumhujumu huyu muhujumu mkuu aliyewatia utumwani.
Kwa ufupi huyo ndiye James Rugemalira tapeli na fisadi aliyeliingiza taifa msambweni anayeendelea kutesa bila kuteseka gerezani. Ni ajabu kuwa juzi rais Jakaya Kikwete aliwahimiza wakuu wa mikoa kuwashitaki wahujumu wa uchumi  lakini akazidi kula na kulala kitanda moja na akina Rugemalira!

No comments: