The Chant of Savant

Saturday 21 December 2013

Kikwete na Pinda wafuatie wawajibike


Baada ya rais Jakaya Kikwete kuwafuta kazi mawaziri wanne kwa kosa la kutowajibika kwenye wizara zao, umefika wakati wa kumwambia naye awajibike. Sababu za kufanya hivyo ziko wazi. Kama mawaziri walifutwa kwa vile watu wa chini yao walifanya madudu, basi na Pinda na Kikwete wawajibike kwa vile hawa mawaziri walikuwa chini yao. Pinda alinukuliwa akisema,“Waheshimiwa wote wanne wamekubali kujiuzulu na kilichofanya walikubali kufanya hivyo ni kwamba vyombo vilivyohusika viko chini ya usimamizi wao.” Nadhani Pinda ametoa jibu la ni kwanini Kikwete naye wawajibike. Kwani uwajibikaji wa pamoja (collective accountability) unawahusu mawaziri tu.
Hata bunge lingeondolewa kwa vile nao wako pale kufanya biashara ya mapenzi kama alivyonakiliwa mmoja wao akisema kabla ya kulazimishwa kufuta kauli yake ili kukwepa aibu zaidi. Kimsingi, Tanzania haina serikali wala bunge bali genge la wahuni na walaji tu. Hivyo wananchi tungesimama pamoja na kuhakikisha tunatoa somo kwa kuwawajibisha wote.
Nangojea kusikia atakachosema Kikwete kuhusiana na mawaziri mizigo ambao ni hovyo kuliko hata hawa waliotimuliwa hasa Balozi Hamis Kagasheki ambaye ameondoka tokana na kugusa maslahi ya wakubwa.

2 comments:

Anonymous said...

Hivi ni kweli hawa ndiyo wabovu pekee....Hospitalini huduma duni uthibitisho Rais wa nchi amegundua huduma za afya ni duni nchini kwake jawabu la tatizo kwake yeye alivyoona ni kwenda ughaibuni. Waziri husika na Afya nini kimetokea kwake.

Je hizo zinasemekana nazo ni wizara zenye Dr....Prof....wa Elimu na weingine nao wanafanya vizuri wakati madudu yote yanafahamika.

Wizara ya fedha nayo kweli imeona hakuna chanzo kingine cha kukusanya fedha zaidi kuwatoza walalahoi kodi ya kumiliki simm card..
Je huyu waziri naye anasifa ya kubaki...Kiufupi huu uwozo ambao umetambaa mwili mzima kama kansa ya damu...suluhisho linatakiwa kufanya maamuzi magumu....

Mfumo mzima uondoke tuanze upya...watu wa wenye maarifa ya kiwango cha juu kabisa katika taaluma ya sayansi ya siasa na uchumi watasema hapo suluhisho watatao suluhisho la kitaaluma

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nimependa na kukubaliana na mfano wako kuwa mwili mzima umeharibiwa na kansa hii. Kwa vile Kikwete ndiye kichwa na Pinda moyo basi waondoke sawa na wanavyotaka kuondoa viungo tu wakati tatizo liko kwenye kichwa na moyo wa mwili husika.