The Chant of Savant

Monday 10 March 2014

Ridhiwani anataka kumdanganya nani?


Mwana wa rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani aliyepitishwa na chama cha baba yake kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze ametoa mpya kuwa akienda bungeni atawafundisha wabunge kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kulalamikia posho za vikao.
Wengi wanjjiuliza: Kama Ridhiwani ana uchungu na taifa ni kwanini hakumuelimisha baba yake kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kulinda raslimali za umma? Kama Ridhiwani ana uchungu na taifa hili,  kwanini hakujitenga na kutumia jina la baba yake kupata huo ubunge anaotaka kutumia kuwafundisha wakongwe kujali maslahi ya taifa ambayo yamehatarishwa na baba yake marafiki zake na familia yake? Je Ridhiwani anataka kumdanganya nani? Je Ridhiwani hajui na kuona kuwa anajidanganya kudhani atawadanganya watanzania kuwa ana uchungu na nchi wakati ni mmojawapo waliofika hapo walipo kwa kuihujumu hiyo nchi anayodai kuwa na uchungu nayo? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

4 comments:

Anonymous said...

Mwl Mhango, kwa kuwa mtaji wa wanasiasa (si hasa) za Bongo ni "bongolala" za wananchi, ninaomba kuhitilafiana nawe kuwa atawadanganya wengi tu. Amekwishaanza kwa kujidanganya mwenyewe.

Unadhani "mradi" wa divisheni dala mantiki yake nini? Kwamba..."kalagha baho..."

Kwa kifupi, hali ya taifa letu ni mbaya sana sana sana.

Tunakoelekea hata hakuna anayefahamu.

Inatisha

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon,
Umeua sina la kuongeza kwa vile niliatetea wasiotetewa so to speak. Je tutaendelea na haya mauza uza hadi lini ndugu yangu?

Anonymous said...

Mwl. Mhango, hali inatisha sana.

Kwa maono yangu, nguvu yoyote ya nje haiwashitui the powers that be pale Bongo.

Kitakachofaa ni lazima vuguvugu lianzie pale pale nyumbani, bila hivyo ni kazi bure. Watu wapate "emancipation" na kujua ni nini stahili zao nk ndiyo kitaeleweka.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ano
Nakubaliana nawe. Sisi tunatimiza wajibu wetu kama rais na wazalendo. Kwa mfano, mimi napiga kelele si kwa sababu naumizwa na mfumo wao. Kama ni kuangalia maslahi binafsi ningejinyamazia hasa ikizingatiwa kuwa niko nje na vitegemezi vyangu. Hata hivyo kama mzalendo naona nina wajibu ili angalau historia siku moja iseme kuwa nilipinga huu ulafi na ufisi unaoendelea.