Friday, 15 August 2014

Maisha bora kwa wote na hali hii hapa

Wanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Kiwalani wakifanya mtihani wao wa kumaliza darasa la saba picha kwa hisani ya IPP media.
Kwa watu walioingizwa mkenge kwa kuahidiwa  `Maisha Bora kwa Wote (MBW) sijui wakishuhudia hali kama hii ambapo watoto wao wanafanyia mitahani yao sakafuni wanajisikiaje? Hapo juu mwanafunzi wa shule ya Msingi Kiwalani Jijini Dar akipokea nakala ya maswali ya ya mtihani wake wa kumaliza darasa la saba toka kwa msimamizi. Kweli huyu anaweza kushinda kuingia kidato cha kwanza? Je haya ndiyo Maisha Bora kwa Wote walioahidiwa au utapeli mtupu? Wakati upuuzi huu ukiendelea, aliyewaahidi yote haya anaruhusu Bunge Maalum la Katiba (BMK) kuendelea na vikao kinyume cha sheria na kuiba pesa ambayo angalau ingeweza kununuliwa madawati,
Hivi hii pesa inayopotea ingeweza kusomesha watanzania wangapi na kupunguza ujinga kwa kiasi gani? Je ingeweza kutibia watanzania wangapi? Je ingeweza kujenga kilometa ngapi za barabara au kuleta lita ngapi za maji?

3 comments:

Anonymous said...

INATISHA TENA DAR RAIS NA MAWAZIRI WAPO HAPO; WATOTO WAO HAWASOMI BONGO NDIYO MAANA HAWAJALI : 2015 WATANZANIA NDIYO UWAMUZI WETU CCM HAKUNA KIONGOZI MWADILIFU HUKO WOTE MAFISADI KILA KUKICHA TUNZO

Anonymous said...

watoto wa Nyerere walisoma Tanzania
Rosemary alikufukzwa muhimbili kwa kufeli wakati baba yake ni rais
leo watoto wa vigogo hakuna anayefeli unategemea nini na wote hupewa nafasi nyeti serikalini au kwenye mashirika ya umma

NN Mhango said...

Anon hapo juu mmenena. Tumegeuka taifa la wachoyo na la hovyo. Kila kigogo anataka ale yeye na ukoo wake hata kama alacho ni damu na nyama ya wenzake. Tumegeuka taifa la mafisi na mafisadi wasio na huruma na watu wasio na hatia. Ni laana kiasi gani. Rejea hata mawaziri kughushi wakaendelea kuula na rais akiwakingia kifua. Wakubwa wanasomesha ulaya na wadogo wanaendelea kukaa sakafuni wakiaminishwa kuwa huu ni ulimwengi na mwongo wa sayansi na teknolojia. Sayansi na teknolojia gani watu kukaa chini?