Sunday, 26 December 2010

Heshima au udhalilishaji!

Ajabu jamaa wanachekelea utadhani ni jambo jema! Au huyu mama kaingia kwenye siasa kupitia viti maalum kufanya kazi hii maalum-kujidhalilisha yeye na wanawake wote duniani.Malawi’s Foreign Minister Etta Banda(on her knees, right) welcomes in style, President Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived in Blantyre for one day working visit yesterday. On the left is Malawi’s Minister of transport and public infrastructure. President Kikwete later held talks with President Bingu wa Mutharika of Malawi who is also the current chairman of African Union AU. The President returned to Dar es Salaam yesterday evening.

Hii nayo tunasemaje ingawa tukio zima lau ninasema kuliko picha ya kwanza?


Picha kwa hisani ya profesa JL Mbele.

11 comments:

Mbele said...

Kuna mila za makabila kadhaa ambazo ziko namna hiyo. Akina mama wanapiga magoti au kuchuchumaa kabisa wakati wa kusalimiana na wanaume wa umri au wadhifa mkubwa zaidi yao.

Kutokana na kulelewa namna hiyo tangu utoto, hisia ya kupiga magoti au kuchuchumaa inatoka ndani na ni ya kweli. Ni sawa na hisia inayotupata tunapokutana mzee sana, tukainamisha kichwa na kumsalimia "shikamoo." Tukishatoa hiyo salamu inavyopasika, tunajisikia raha ndani ya nafsi yetu.

Basi na hao wanawake wanaotoka katika tamaduni hizo ni hivi hivi. Ukiwangalia huyu mama hapo kwenye picha, utaona naye amefurahi.

Hilo nililosema hapa juu ni suala la mila kwa ujumla. Lakini labda tujaribu kutafakari zaidi hii picha. Bahati mbaya hatuna namna ya kuingia kichwani mwa huyu mama na kuona alikuwa na fikra gani katika kumpigia magoti JK.

Sina hakika kama mama mwenye wadhifa kama huu anampigia magoti hata mlinzi wa ofisi yake, au dereva wake, hata kama mwanamme huyu ni mzee zaidi.

Kwa hivi, najaribu kuwazia hii picha, na nahisi kuwa labda kilichomsukuma huyu mama ni kuwa JK ni mwakilishi wa taifa la Tanzania. Kwa hivi huenda kilichotawala kichwani mwa huyu mama ni wazo la kutoa heshima kwa Tanzania.

Hata mimi niko tayari kupiga magoti kwa heshima ya nchi yoyote. Kwa maana nyingine, nikiiona bendera ya Malawi nikajawa na hisia ya kutoa heshima kwa nchi ile, niko tayari kupiga magoti. Iwapo dhamira yangu itakuwa ni kutoa heshima kwa nchi, nitafanya hivyo hata mbele ya rais wa nchi ile. Mawazoni mwangu sitakuwa namfikiria yule mtu, bali nchi.

Huenda haya ndio yaliyokuwa kichwani mwa huyu mama alipopiga magoti mbele ya JK.

Hata hivi, napenda kutoa ufafanuzi. Kupiga magoti mbele ya bendera ya nchi hakuna utata. Na kama rais wa nchi kweli ni mwakilishi na kielelezo cha nchi, kwa maana halisi ya kuwa ni mzalendo kweli, na kielelezo cha heshima ya nchi, naona ni ruksa kumpigia magoti.

Sasa basi, ili JK astahili kupigiwa magoti namna hii, ingebidi awe ni kweli mwakilishi wa nchi yetu, kielelezo bora cha uzalendo na heshima ya nchi yetu, kama ilivyo bendera yetu, au kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere.

JK wa leo si yule niliyemwelewa pale mwanzoni, yaani mwaka 2005. JK wa leo amejidhihirisha kuwa hana mpango wa kuitukuza nchi yetu kikamilifu. Anavyolichukulia suala la ufisadi ameweka dosari. Vile vile, mchakato uliomweka kwenye urais awamu hii una walakini. Haukuwa na uwazi, ukweli, na haki kwa kiwango ninachotegemea.

Kutokana na walakini huo, mimi ingawa niko tayari kuipigia magoti bendera ya Tanzania, siko tayari kumpigia magoti JK. Bendera ya Taifa haina dosari, wakati CCM imeutia dosari mchakato uliomweka JK katika urais. Kwa maana hiyo, urais wake una dosari. Ni rais halali kisheria, lakini kuna dosari kwenye suala la haki.

Kwa hivi, ningekuwa nimepata fursa ya kushauriana na huyu mama kabla, halafu labda nikajua kuwa lengo lake ni kutoa heshima kwa Tanzania, ningemwomba asipige magoti mbele ya JK, ila labda asogee tu kwenye bendera ya Tanzania, akapige magoti hapo kwenye bendera, kama lengo lake lilikuwa ni kutoa heshima kwa Tanzania, ili heshima hiyo itue panapostahili.

Kwa leo, ngoja niishie hapa, ingawa naelewa kuwa suala hili ni tata, na tunaweza tukasema mengi sana.

NN Mhango said...

Kaka Mbele,
Nakubaliana nawe kuwa Kikwete hana hadhi ya kupigiwa magoti. Pia nakubaliana nawe kuwa bendera ya Tanzania, kama ni heshima, basi ndiyo inastahili kufanyiwa hivyo. Napingana nawe. Hakuna binadamu binadamu apaswaye kupigiwa magoti hata awe Nyerere, Mandela, Yesu, Mohammad, Mkwawa wala nani. Hizi ni mila zilizopitwa wakati na ni ushirikina kwa lugha nyepesi. Hii haina tofauti na kutoa sadaka kwa vinyago au kuviabudia. Haina tofauti na kutupia mawe minara na madudu mengine kama hayo au kubusu mawe. Hii ni shiriki kwa lugha nyepesi.
Laiti Kikwete angekataa heshima hii ya kizamani inayokinzana na usawa wa binadamu. Kwanini yule waziri wa uchukuzi aliye jirani hakumpigia magoti Kikwete. Nadhani kupiga magoti kusingebagua jinsi nisingekuwa nao ugomvi.

Mbele said...

Kama nilivyosema, hili suala ni tata sana. Kwa upande moja, binadamu wote wanaishi kwa kutumia ishara. Kuzaliwa na kukulia katika utamaduni fulani ni mwanzo wa kujifunza ishara za utamaduni huo.

Kwa mfano, tunapokutana, tunasalimiana kwa maneno na kushikana mikono. Ishara hii ya mikono ni wajibu. Mtu akinyoosha mkono, unategemewa kumnyooshea mkono pia, sio mguu.

Ukienda kwa wakwe, kutegemeana na utamaduni husika, utabeba jogoo au kibuyu cha mbege. Kwenye mila zingine, wachumba au wana arusi wanavalishana pete. Siku nzima na maisha yetu yote, tunatumia ishara za utamaduni wetu.

Ishara na sherehe ni uhai wa kila utamaduni, na hazikwepeki. Angalia jinsi hapo juu tunavyokubaliana kuhusu bendera ya Taifa. Bendera ni ishara mojawapo, na tunaikubali. Mtu akiidharau, akatumia bendera ya taifa kupangusia viatu vyake, wewe na mimi tutamshughulikia ipasavyo.

Hii mila ya kupiga magoti nayo ina mengi ambayo bado hatujayagusia. Inaweza kuandikiwa hata kitabu. Kwa mfano, mwangalie jamaa huyu hapa

NN Mhango said...

Kwa picha kiambatanisho umeniacha hoi ingawa tukio lau linaweza kutoa ujumbe moja kwa moja kuliko ya kwanza. Hapa tunaona bwana harusi akipiga goti nadhani hampigii goti bi harusi bali kujiandaa kumbeba. Hapa unaweza kuniuliza ni kwanini bi harusi huwa hambebi na kumbembeza kindayaya bwana harusi. Nadhani maumbile yetu yanasema zaidi ya tunavyoweza kuhoji au kutoa maelezo.
Picha yako naitundika kama ilivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Mimi naamini hakuna kabisa udhalilishaji katika kupiga magoti kwa mtu unayemuheshimu ila kama utakuwa umelazimishwa hapo ndio. Hii habari/mila kwangu sio ngeni kabisa na wala sioni kama ni unyanyasaji. Kule kwetu ungonini tunapiga magoti kwa waliotuzidi umri, wakwe nk. nakumbuka mara ya kwanza kabisa bibi yangu mzaa mama alikuwa akimwona baba anampigia magoti na ukapulya wangu nikamuuliza kwanibni anafanya hivyo? akasema ni mila na pia ni heshima tu.
Na baada ya miaka nikahamia ubenani hapa ndo nilipoona jinsi upigajimagoti ulivyo yaani we acha tu yaani wabena wana jua kupiga magoti bwana wewe. Lakini mimi sioni ni kitu cha unyanyasaji ni mila na ni utamaduni. Kumbuka huku kupiga magoti hata wenzeti hapa kale walikuwa wanapiga magoti na sasa kunaanza ku├ąpotea na kuanza kukumbatiana. Na sasa naona kama kawaida yetu nasi tunajifanya kuiga kuacha kupiga magoti.

Mzee wa Changamoto said...
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaa
Suala la KUDHARAULIKA ama KUNYANYASIKA KIJINSIA halijawahi kutokana na KITENDO, bali TAFSIRI na HISIA ya kile kitendekacho.
Lakini suala la HESHIMA ama NIA ya kufanya ufanyalo yaweza kuwa kigezo ha HESHIMA ama DHARAU. Kuna wakati ambao kumheshimu asiyestahili (hata kama unadhani ni sahihi) kunaweza kutafsiriwa kama dhalilisho.
Sina hakika kama huyu Mama alifanya haya akifuata tamaduni ama akiamini kuwa Rais Kikwete anastahili HESHIMA HIYO.
Unadhani wanaosema wanadhalilishwa "kupigishwa" magoti hawapi(ga)gi nyakati nyingine wapendazo wakifanya wapendayo?
WANAFANYA
Je! pale WAHITAJIKAPO kupiga magoti (kama kwenye kuchota maji nk) unadhani wanahisi kunyanyasika?
LA HASHA!!
Si kwenu ukimpiga mkeo unamnyanyasa kijinsia? Huku nje ya nchi je? Lakini kwa yale makabila ama sehemu waaminio kuwa hicho ndio kigezo cha wivu unaoakisi kiasi cha upendo...SI WANAONA NI BARAKA KWAO?
Kwani hatuoni kuwa kuonesha alama ya dole gumba ni ishara kuwa kila kitu kiko swafi, je nchi za Iraki na Irani wanalichukuliaje?
Ama hujaona wanaosalimiana kwa kuoneshana "kidole cha kati" (japo kwa mizaha) ilhali ukiwatendea wewe msiyetaniana mnaweza kutoana ngeu.
Amaaaaaaaaaaa...Si kote ni KUPIGA MAGOTI ama ni KUMPIGA MWANAMKE ama ni KUMNYOOSHEA KIDOLE CHA KATI?
Kwanini basi tafsiri ya KUONEA ama KUDHALILISHA ama KUNYANYASA isiwaguse wengine ama walewale kwa namna moja na iwaguse kwa namna nyingine?
Ni kwa kuwa NAMNA TUONAVYO TATIZO NDILO TATIZO.
Kuna mengi (hasa yafanyikayo nyuma ya pazia na zaidi kwa wanandoa) ambayo kwa hakika yakitendeka kwingine ama yakisemeka utendekaji wake ni KUNYANYASIKA, lakini yakitendwa kwa yatendwavyo na kubaki kwa watendayo, ni chachandu ya mapenzi

NAACHA...Tuonane NEXT IJAYO

NN Mhango said...

Da Yacinta umeniacha hoi ingawa sikubaliani na uoni wako juu ya hili. Nadhani mila wakati mwingine huwa kama dini.They are more dogmatic than logical. Sishangai kuona kwa mfano mnigeria wa Jos akiaminishwa kuwa kumuua mkristo ni njia ya kwenda peponi ingawa siyo. Hivyo nitalazimika kukubaliana nawe kwa vile kama mwanamke umeridhia hilo.
Mzee wa Changamoto kweli umetoa changamoto. Kimsingi nimekuelewa kuwa kila kitu ni relative. Pamoja na uoni huo, tunakubaliana kitu kimoja-ushuzi hunuka hata uitwe manukato. Hapa hakuna cha relative or what. Ushuzi ni ushuzi. Samahani ashakum si matusi kwa kuutaja kama ulivyo ingawa ndivyo ulivyo. Ushuzi ni ushuzi na udhalilishaji ni udhalilishaji. Nitoke nje ya mada. Kwa mfano, kwanini kuna vitu maalum kwa akina mama si kwa akina baba? Je huu nao licha ya kuwa wizi wa pesa ya mlipa kodi si udhalilishaji na ucheleweshaji wa kina mama?

Tukirejea kwenye picha ya hapo juu ya Malawi, je hapa kinachopigiwa magoti ni binadamu au urais? Kwenye sebule ya Matondo kuna picha ambapo mama mmoja anampigia magoti mke wa Kikwete. Je kinachopigiwa magoti hapa ni Salma au first lady? Tafakarini na asanteni kwa michango yenu. Nategemea kusikia zaidi toka kwenu.

Anonymous said...

Naweza kusema kuwa kuna mila za kitanzania za kupiga magoti kumsalimia mkubwa. Lakini sio kuweka goti kabisa chini au kutambaa.Lakini hii nadhani imezidi jamani... Ktk maisha yangu ninapiga magoti kumuomba Mwenyezi Mungu na sio kumpigia binadamu.

Mucherino said...

Da Yacinta umeniacha hoi ingawa sikubaliani na uoni wako juu ya hili. Nadhani mila wakati mwingine huwa kama dini.They are more dogmatic than logical. Sishangai kuona kwa mfano mnigeria wa Jos akiaminishwa kuwa kumuua mkristo ni njia ya kwenda peponi ingawa siyo. Hivyo nitalazimika kukubaliana nawe kwa vile kama mwanamke umeridhia hilo. Mzee wa Changamoto kweli umetoa changamoto. Kimsingi nimekuelewa kuwa kila kitu ni relative. Pamoja na uoni huo, tunakubaliana kitu kimoja-ushuzi hunuka hata uitwe manukato. Hapa hakuna cha relative or what. Ushuzi ni ushuzi. Samahani ashakum si matusi kwa kuutaja kama ulivyo ingawa ndivyo ulivyo. Ushuzi ni ushuzi na udhalilishaji ni udhalilishaji. Nitoke nje ya mada. Kwa mfano, kwanini kuna vitu maalum kwa akina mama si kwa akina baba? Je huu nao licha ya kuwa wizi wa pesa ya mlipa kodi si udhalilishaji na ucheleweshaji wa kina mama? Tukirejea kwenye picha ya hapo juu ya Malawi, je hapa kinachopigiwa magoti ni binadamu au urais? Kwenye sebule ya Matondo kuna picha ambapo mama mmoja anampigia magoti mke wa Kikwete. Je kinachopigiwa magoti hapa ni Salma au first lady? Tafakarini na asanteni kwa michango yenu. Nategemea kusikia zaidi toka kwenu.

Liz Wallace said...

Da Yacinta umeniacha hoi ingawa sikubaliani na uoni wako juu ya hili. Nadhani mila wakati mwingine huwa kama dini.They are more dogmatic than logical. Sishangai kuona kwa mfano mnigeria wa Jos akiaminishwa kuwa kumuua mkristo ni njia ya kwenda peponi ingawa siyo. Hivyo nitalazimika kukubaliana nawe kwa vile kama mwanamke umeridhia hilo. Mzee wa Changamoto kweli umetoa changamoto. Kimsingi nimekuelewa kuwa kila kitu ni relative. Pamoja na uoni huo, tunakubaliana kitu kimoja-ushuzi hunuka hata uitwe manukato. Hapa hakuna cha relative or what. Ushuzi ni ushuzi. Samahani ashakum si matusi kwa kuutaja kama ulivyo ingawa ndivyo ulivyo. Ushuzi ni ushuzi na udhalilishaji ni udhalilishaji. Nitoke nje ya mada. Kwa mfano, kwanini kuna vitu maalum kwa akina mama si kwa akina baba? Je huu nao licha ya kuwa wizi wa pesa ya mlipa kodi si udhalilishaji na ucheleweshaji wa kina mama? Tukirejea kwenye picha ya hapo juu ya Malawi, je hapa kinachopigiwa magoti ni binadamu au urais? Kwenye sebule ya Matondo kuna picha ambapo mama mmoja anampigia magoti mke wa Kikwete. Je kinachopigiwa magoti hapa ni Salma au first lady? Tafakarini na asanteni kwa michango yenu. Nategemea kusikia zaidi toka kwenu.