Monday, 20 December 2010

Je ingekuwa kweli dunia ingekuwaje? Tafakari




Je hayawani huyu kweli angepata bunduki angelipiza kisasi kwa wanaomuweka kwenye orodha ya viumbe walio kwenye hatari ya kutoweka? Je angeitumia kihayawani kama binadamu au kibinadamu kama hayawani? Je angeitumia kibinadamu japo hayawani? Je yawezekana siku moja hayawani akawa na uwezo na akili ya kumudu zana hii? Je ingekuwa kweli dunia ingekuwaje? Hivi huyo jamaa hapo juu na akina Laurent Gbagbo,Robert Mugabe,Saddam Hussein, Omar Bashir na wengine kama hao nani bora?

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kwani kuna tofauti gani kati ya binadamu na huyu? Huyu pengine hata akimudu kuitumia silaha hii ataitumia kwa kujitafutia chakula chake tu na si vinginevyo. Si kama binadamu ambaye anaweza kuua kwa ajili ya kujifurahisha tu...na hata kujilimbikizia mali za wizi kupindukia huku akiwaacha binadamu wenzake wakifa na njaa!

Binadamu anaweza kuwa mnyama kuliko wanyama wengine wote!!!

NN Mhango said...

Ulosema mkuu mwenzangu ni kweli. Na wala sina nyongeza zaidi ya kusisitiza kuwa binadamu ni mnyama kuliko mnyama.