Monday, 6 December 2010

Ya Pinda na kukataa shangingi na hiyo katuni vipi?
Madili ndani ya maadili.

Katuni ni kwa hisani ya IPP Media.Waziri mkuu Mizengo Pinda huwa haishiwi vituko na mizengwe. Aliwahi kukoromea matumizi mabaya ya raslimali na fedha ya umma bila kuchukua hatua yoyote zaidi ya kulalama.
Aliwahi kutangaza 'umaskini' wake wakati bosi wake na wenzake walikula jiwe.

Juzi kaja na mpya ya kufungia mwaka alipokataa shangingi lenye thamani ya shilingi 280,000,000. Ajabu ya maajabu alikaririwa akisema kuwa hakuhusishwa kwenye mchakato wa kununua dude hili hatari. Hivyo alilikataa kwa madai kuwa alilo nalo bado linadunda mzigo. Je kukataa kukataa tu ni jibu au kutafuta umaarufu? Kama yeye ndiye mwenye dhamana ya kuidhinisha au kutoidhinisha ununuzi wa magari, alizuiliwa na nini kuamuru lirejeshwe huko lilikolanguliwa na kurejesha 'chenji' yetu?
Je anamlalamikia nani iwapo yeye ndiye mwenye mamlaka? Je mamlaka yake ni ya kazi gani?
Je, kwa mantiki haya, Pinda achukuliwe kama shujaa, mzalendo na mwajibikaji au?

6 comments:

Subi said...

Siasa ilivyojaa vituko, visa na mikasa, ukiketi kuwasikiliza hao na kuwashabikia, walahi utaishia kula ugali wa kurumang'ia na wanao wakuone chizi.

Watu hawa husema kama wehu wakati mwingine, na hufanya mambo ya ajabu mara nyingine ambayo mawazo yao huhitilafiana na mioyo yao. Wapo wanye aibu na wapo wanaofunika kombe mwanaharamu apite kujifanya hawajaona.

Angetumia mamlala aliyonayo kukataza magari yote yaliyonunuliwa kwa 'vijisenti' hivyo, ningemweka katika kundi la wanaopigania mali ya umma, alichofanya sawa na alichoniambia mdogo wangu Enson, "kumwaga debe la sukari baharini ukitaraji maji yawe matamu"...

nakopho mleu! (kwa heri ndugu).

Anonymous said...

Alichofanya Pinda ni kutaka sifa au kuonyesha wazi asivyo na ubavu. Sisis tunaofanya kazi serikalini tunajua mengi yanayohusu matumizi mabaya kuliko hata hili. Wanauziana magari kama hayo kwa chini ya shs ten million. Ni hatari kama mwananchi wa kawaida akijua na kuamua imetosha.

Malkiory Matiya said...

Pinda Mizingo, I Malkiory William Matiya as for this date of 7/12/2010, annoint you as a true son of Tanzania and for sure you belong a peasantary class!

Anonymous said...

Mkulima halisi huyu hana makuu hata trekta akipewa atatumia na yeye ni waziri.

NN Mhango said...

Da Subi na Melkior mmemaliza yote. Laiti wadanganyika wote angalau nusu wangekuwa hata na robo ya uchungu na usongo wenu kwa taifa, basi tungekuwa mbali aminini.
Anonymous namba moja na mbili nawashukuruni pia kwa uoni wenu ingawa wengine sikubaliani na uoni wenu.
Kila la heri na karibu tena kwenye sebule hii.

Anonymous said...

Anafanya mchezo wa kuigiza tu. Mi nafikiri akili zake zimePinda na zimejaa Mizengwe kama jina lake!! Kwa nini angalau hakuagiza hilo gari lirudi liliko toka ili akaunti yake ikamilike?