Wednesday, 8 December 2010

Waweza amini haya ni majeneza?Dunia haiishi vituko. Vituko vingine huchekesha, kufundisha hata kufikirisha wakati vingine humuacha mtu asijue la kushika!
Nchi ya Ghana huwa nayo haiishiwi vituko. Ina makabila yenye majina mafupi kama Ba, Ga, Ma na mengine mengi.

Ni katika taifa hili ambapo kifo uheshimiwa kuliko uhai. Ni katika sehemu hii ya dunia ambapo mamilioni ya fedha hutumika kwenye mazishi badala ya maisha. Hivyo, usishangae kumsikia mghana akidunduliza kwa ajili ya mazishi badala ya mambo mengine.

Kuongeza utamu kwenye hili, waghana huzikwa kwenye majeneza yanayowakilisha kazi, wadhifa na mapenzi ya marehemu. Rubani huzikwa kwenye kaburi mfano wa ndege, dereva, gari, mlevi chupa na mengine kama hayo.
Siachi kujiuliza. Watu kama Casanova, Osama bin Laden, wezi wetu wa EPA na Richmond wangezaliwa nchini Ghana wangezikwa kwenye majeneza ya namna gani?

Na kama wewe ulikuwa mpayukaji, ungezikwa kwenye jeneza mfano wa nini? Tafakarini.


wezi wa epa
bin laden

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Nadhani kufungwa kwenye tambara za miti ya kwetu bado ni the best.
Lol!!!!!!!!!!!!!
Ila majeneza mengine haya??? Niliona(ga) moja iliyo kama benz na kwenye boneti / hood ndipo panapofunuliwa ili kuonesha mwili wa marehemu