Tuesday, 7 December 2010

Ni watanzania waishio nje au mapandikizi ya CCM?
Kutoka Kushoto ni Katibu wa Uchumi, Mipango na Fedha wa Tawi Boniface Assenga anayefuatia ni Mwenyekiti wa Tawi Dk. Alfred Kamuzora akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Tawi Neema Kengese na anayefuatia ni Salim Mfungahema Katibu wa Siana, Sera na Uenezi wa Tawi (Moscow Urusi)

Kila mara nimekuwa nikisoma habari za 'watanzania' wanaoishi nje kusherehekea uhuru wa Tanzania, kumpongeza Kikwete na mambo mengine mengi ingawa sijawahi kuwasikia wakishinikiza kupata haki ya kupiga kura.
Maarufu ya jumuia ambazo nimeishasoma habari zao hasa katika kumpongeza Kikwete ni zile za Watanzania waishio Urusi, Italia na Japan kwa uchache tu.

Je inakuwaje watanzania waishio nje na jumuia zao ziwe karibu na CCM tu na si vyama vingine? Je hawa ni wawakilishi wa watanzania waishio nje au mapandikizi ya CCM na wale waliofadhiliwa na CCM kuwa nje?
Mabalozi wa nchi za kiswahili hawana utaratibu hata wa kukusanya takwimu za raia wao walioko nje ukiachia mbali mmoja balozi Maajar wakati alipokuwa Uingereza.
Tusaidieni. Kwanini jumuia nyingi za wabongo zilizoko ughaibuni zinaonyesha kujikomba kwa watawala wanaoshiriki na kulea ufisadi? Je nao hawoni kama hao wanaowaabudia?

4 comments:

Anonymous said...

If you ask me they are all damn stupid period.

Anonymous said...

Wote huwa ni wababaishaji wanaotafuta gear ya kuingilia kwenye utawala haramu ili nao wapate nafasi ya kuifisidi nchi yetu. Wapo huko lakini wanatamani vitu fulani vinavyotokea nyumbani.

Anonymous said...

These guys are goons. They are just like dogs that can lick anybody's ass.
We need to stand in their way before they make it. Fuck them wherever they are.

Anonymous said...

Wengi ukisoma majina ya ubini wao, ni wale watoto wa viongozi waliopo serikalini au waliostaafu au walotutangulia. Mtoto wa mkulima apate wapi nafasi ya kuongea mambo ya CCM. Vijijini hakuna radio ndo maana watu wanadhani Nyerere bado kiongozi. Watendaji wa vijiji au mabarozi bado wanawadanganya vizee eti nyerere kasema msichague wapinzani. Wale wenye uelewa, kadi zao za kupiga kura lazima zitakuwa na matatizo au watapewa sababu za kutopiga kura. Iweje jimbo moja wapiga kura 40% wasipige kura????

hao mlio nje na mnaishabikia CCM, jiandae kufirisiwa mali zenu mlizogawana na hao mafisadi wenzenu. Saa ya ukombozi yaja.

Mtoto wa mkulima.
CCM