Tuesday, 14 December 2010

Zuma amshitaki mchora vibonzo
Nchini Afrika Kusini hali si shwari. Tuhuma za ubakaji na ufisadi zinazidi kumuandama rais Jacob Zuma. Jinamizi la kashfa za Zuma lilifufuka hivi karibuni Zuma alipoamua kumshitaki mchora vibonzo maarufu nchini mle, Jonathan Shapiro.

Kibonzo cha Shapiro kijulikanacho kama Zapiro hapo juu kilitoka miaka miwili iliyopita kikionyesha jinsi Zuma alivyotumia madaraka na ushawishi wake kuzima haki za mwanamke aliyedaiwa kumbaka.
Je hatua ya Zuma inaimarisha au kudhoofisha uhuru wa vyombo vya habari? Je Zuma ataendelea kuitumia mahakama iliyojaa wateule wake kuendelea kuukimbia mzuka wa jana yake? Hadi lini?

Pamoja na kudaiwa jumla ya $ 731, 000 kama fidia, Shapiro anasema kupitia wakili wake:"Nadhani rais ameshauriwa vibaya. Watakachofanya yeye na timu yake ni kurejesha kesi hii kwenye jicho la umma."

Alikaririwa akisema Eric van der Berg anayemtetea Shapiro na gazeti la Sunday Times. Je Zuma ataendelea kujivua nguo mwenyewe au kunywea? Time will surely tell.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!!
Hii kali. "Kashikiwa"?
Kumbe ndio alivyo?
Hahahahaaaaaaaaaaa. Sikuwahi kuiona hii. Kaazi kwelikweli