How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Wednesday, 5 January 2011
Siku Kikwete alipoandaa safari yake ICC The Hague
Josephine Slaa akibubujikwa damu baada ya kujeruhiwa na polisi
Damu imemwagika Tanzania kwa mara nyingine. Kipindi si kule Zanzibar bali Bara ambako kulidhaniwa kunakaliwa na "makondoo."
Rais aliyerejea madarakani kwa wizi wa kura wa Tanzania Jakaya Kikwete, amejiongezea sifa nyingine ya uuaji. Wachambuzi wa mambo watakubaliana nasi kuwa serikali ya Kikwete licha ya kuuibia umma kura na fedha, sasa imefungua ukurasa mpya wa uimla na umwagaji damu.
Kosa lililotendwa na watanzania maskini eti ni kudai haki yao ya kuzuia Kikwete na genge lake wasiendelee kuwaibia.
Tarehe 5 Januari 2011 inaingia kwenye kumbukumbu chafu za taifa letu. Kwani ni siku, kwa mujibu wa taarifa toka kwenye tukio mjini Arusha, ni kwamba watu wasiopungua kumi wameauawa na mamia kujeruhiwa na polisi waliotumwa na Kikwete kuzuia maandamano ya kupinga wizi wake na genge lake linalotumia kampuni ya Dowans kutaka kujipata jumla ya shilingi 185,000,000,000 just kwa kuwahujumu watanzania. Pia mali zenye thamani ya mabilioni zimeharibiwa.
Taarifa zinasema polisi wamefyatua risasi kwa siku nzima na kupasua mabomu ya kutoa machozi kwa siku nzima kupambana na waandamanaji wanaotaka viongozi wao waachiwe.
Ni genge hili hili ambalo chini ya kampuni mama wa Dowans ya Richmond liliweza kuiba mabilioni ya fedha kwa kujilipa jumla ya shilingi 152,000,000 kwa siku kwa miaka miwili. Kwa kipindi hiki kifupi genge hili lilifanikiwa kuubia umma wa watanzania maskini jumla ya shilingi 110,656,000,000.
Kumbuka. Ni genge hili likiongozwa na Rostam Aziz na Edward Lowassa liliasisi,kwa ya msaada mkubwa wa Benjamin Mkapa,lilivunja Benki Kuu na kufanikiwa kuiba mabilioni ya shilingi yaliyotumika kumuingiza Kikwete madarakani. Mchovya asali hachovyi mara moja. Baada ya Kikwete na genge lake kunogewa, waliasisi wizi mwingine ambao umesababisha umwagaji damu na ukatili wa ajabu siku tajwa.
Kumbuka. Siku chache kabla, mtandao wa Wikileaks uligundua wizi mwingine kwenye ununuzi wa rada na kukwama kununuliwa ndege tano zilizopaswa kufufua Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) lililouawa na serikali fisadi.
Wengi wanajiuliza. Kwa kosa hili dhidi ya ubinadamu Kikwete ataukwepa mkono mrefu wa sheria wa Mahamaka ya Kimataifa ya The Hague inayoongozwa na mwendesha mashitaka wake machachari Louis Moreno-Ocampo ambaye amewasambaratisha vigogo nchi ya jirani ya Kenya?
Baada ya katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais anayeaminika kushinda kwenye uchaguzi ulioibiwa lakini akaibiwa ushindi Dk. Wilbroad Slaa kutoa madai kuwa nyuma ya Dowans kuna Kikwete, Kikwete alipandishwa hasira kiasi cha kuamuru mauaji haya ya halaiki. Je amani ambayo Kikwete na waramba viatu wake wamekuwa wakiimba sasa iko wapai? Za mwizi ni arobaini na Mungu hamfichi mnafiki. Sasa Kikwete na uchafu wake yuko uchi mbele ya mataifa kuona.
Tunahimiza watanzania kutotishwa wala kukubali yaishe. Waandamane na kujitoa mhanga kuhakikisha genge la majambazi wenye madaraka linatimuliwa kama siyo kufikishwa The Hague. Hakika SAA YA UKOMBOZI ni hii.
Kikwete amejitengenezea mwenyewe waranti ya kwenda The Hague kuungana na wenzake kina Charles Taylor na Omar Bishkir Bashir.
Kuna maswali muhimu yanayopaswa kujibiwa na watanzania:
1. Kweli Tanzania ni nchi ya amani na utulivu au woga tu na kutokuwapo mapigano ya bunduki?
2. Je kipindi hiki Kikwete aliyenusurika Februari 2008 kwa kashfa ya Richmond baada ya kumtoa kafara swahiba yake Lowassa, atanusirika?
3. Je watanzania watanywea mbele ya ubabe na ufisadi wa wazi wa Kikwete na genge lake?
4. Je watanzania wataridhia kuendelea kunyanyaswa na jeshi la polisi ambalo linaendeshwa kwa kodi zao?
5. Je watanzania wamefikia wakati na mahali pa kusema enough is enough?
6. Je Kikwete atakuwa kichwa ngumu na mpuuzi kuendeleza ubabe na mauaji akijua ICC imeishatandaza nyavu zake Afrika?
7. Je mafisadi kwa kutumia serikali yao ya kifisadi wataendelea kuibia nchi huku wananchi wakiendelea kusota?
8. Je Kikwete ameamua kufa na mafisadi hata kwa kuhatarisha usalama wa nchi?
9. Je jeshi la polisi litaendelea kujirahisi na kutumiwa kama nepi na akina Kikwete kuwapiga ndugu na jamaa zao wanaodai haki zao?
10. Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Kikwete? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Kama mpiganiaji haki za binadamu, nashauri umma usimame kidete na kujikomboa vilivyo kutokana watawala wezi na woga wanaoiba kodi na kuitumia vibaya kulipa majeshi yao kandamizi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Hii mantra ya "amani na utulivu" imeishia wapi? Lakini maharamia wote ndio walivyo.
Tanzania hakuna amani bali imani ya amani. Hivyo mantra ya amani na utulivu ni uongo na ujambazi wa kawaida ndugu yangu. Nadhani sasa kilichokuwa nyuma ya pazia kimefichuka ili kila mmoja ajionee.
Mimi nashindwa kuelewa, Je wale cuf walioandamana juzi mbona hawakupigwa wala kushitakiwa? au waliachiwa wapite kinyemela makusudi ili watu waseme wao ndo waliobua hisia za katiba mpya? Kwanini polisi watumie silaha za moto kwa cdm jamani? yaani raia anafanyiwa sawa na jambazi anavyofanyiwa? Kama walivunja sheria si wangekamatwa kwanini wapigwe na kujeruhiwa? Roho inaniuma sana,ila sina sauti ya kuwatetea watanzania zaidi ya sala tu.Mimi ni mwan ccm lakini hawa polisi wanavyofanya mimi vinanisikitisha sana, wao ndo wanavuruga amani ya nchi yetu.
Polisi wetu ndiyo majambazi wakubwa. Mabosi wao ndiyo usiseme. Tanzania tunatawaliwa na majambazi wakitumia maguvu kuendelea kutuibia. Kuna siku kitaeleweka.
Mimi najiuliza tena na tena hivi huko CCM hakuna mtu mwenye busara aliyebaki kumwambia huyu mtu "STOP"? Kama wanamuogopa ni kwanini? CCM wajiulize tena na tena pamoja naku-plant picha mbaya kwa wapinzani mbona wapinzani wanaendelea kuchukua viti vya Umeya mikoani or kuchaguliwa na wananchi? Mimi sina chama nachagua mtu kutokana na sifa sio chama. Lakini siwezi kumuamini mtu ambaye yuko madarakani for all those years anaimba maji safi, umeme, afya na elimu hajaweza fanikisha chochote mpaka sasa na wala hamna dalili za improvement. Kikwete na wenzio mpaka mtakapofanya vitu kwa vitendo ndio watu watawaelewa lakini zaidi ya hapo ni vurugu tu. Kwani kunashida gani yakuwa na transparency kwenye government kama kila kitu kinafuata sheria? Kwanini Kikwete na wenzako hamueleweki mara Richmond, mara Epa, mara Dowans mmiliki hajulikani mara bei zimepanda etc. Hivi kweli huyu mtu ana-plan yeyote anaifuata? Are there any priorities in your table Mr. President? Kwakweli hebu tuwekeni amani yetu pembeni tusiwe wajinga kiasi hiki maandamano ni lazima, maswali ni lazima, debates ni lazima mpaka tuelewe how we get here, who is involved and where are we going from here? Mtanzania yeyote ulipo do your best kuikomboa tanzania kwa mawazo, shinikizo,vitendo, tuma picha za Arusha kwenye different free media e.g. Aljazeera, CNN etc. Kama unaweza tengeneza documentary weka kwenye You tube millions waweze kuona what is going on, Elimisha watu kwenye eneo lako kazi ya government na viongozi ni kuwatumikia na sio kuwatawala, waelewe madai yao na wasiwe waoga etc Tutafika tu I guarantee you all! We need to keep on squeezing them real hard!!!
Post a Comment