How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Sunday, 23 January 2011

Je watawala wezi na mafisadi wa Kiafrika husoma haya?


Hekalu la fashisti Mobutu Seseseko wa DRC iliyoko Monaco

Hekalu la dikteta Theodor Obiang Nguema wa Equatorial Guinea liliko Malibu


Hekalu la Omar Bongo mwizi wa zamani wa Gabon lililoko Paris na ni moja kati ya 33 aliyokuwa akimilki.








Hivi karibuni shirika la habari la Uingereza (BBC) liliripoti kisa hiki hapa chini kama kilivyo bila kuongezewa wala kupunguzwa.

Hii ni siku chache baada ya mabenki nchi Switzerland kutangaza kuzuia akaunti za dikteta wa zamani wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali.

Kasri hili la bei mbaya (chateau) ni mali ya dikteta wa zamani wa nchi maskini kabisa ya Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa ambaye naye alikufa maskini baada ya kufuja chumo la wizi. Alifia gerezani akiwa kapuku hakuna mfano. Umaskini ulimchoma hadi akajirejesha mwenyewe kama alivyofanya dikteta wa zamana wa Haita Jean Claude Duvallier maarufu kama Baby Doc.

Je ni wezi wangapi walioko madarakani wana mali kama hizi huko Ulaya zikingoja kufichuliwa na kutaifishwa baada ya kupigwa teke na wimbi la mapinduzi ya nguvu ya umma linalozidi kupata kasi barani Afrika?

Kwa habari zaidi soma habari hii hapa chini.



African dictator Bokassa's chateau sold at auction




A French chateau that once belonged to African dictator Jean-Bedel Bokassa has sold for 915,000 euros (£760,000).

The dilapidated 'Chateau d'Hardricourt' was bought by an anonymous bidder at an auction in Versailles.

Bokassa spent several years living in the mansion in the western Paris suburb of Hardricourt after he was overthrown as leader of the Central African Republic (CAR) in 1979.

It has since fallen into disrepair and needs major refurbishment.

"Electricity, water, heating - all need to be overhauled," Pascal Koerfer, lawyer for the administrator of the Bokassa estate, told Associated Press.

The property overlooking the Seine comes with 10,000 square metres (108,000 sq ft) of surrounding parkland, a house for a caretaker and a double garage.

But Mr Koerfer estimated it would take up to 3m euros (£2.5m) to restore it to a "liveable" condition.

More than 80 potential buyers are reported to have viewed the property before the sale.
'Lamentable' state

One curious visitor, described only as Marcel, told Europe 1 radio network that the chateau was in a "lamentable" state: "The manor is not heated, there are broken windows and ceilings falling in."

The chateau was occupied by one of Bokassa's wives and two of his children up until a few years ago. One of the daughters, Marie-France, is quoted as saying they did not have the money to maintain the property.

One of Bokassa's sons, Georges, who was at the auction, had urged French President Nicolas Sarkozy to intervene to prevent what he called the plundering of his family's heritage.
Former Central African Republic ruler Jean-Bedel Bokassa poses with seven of his children at 'Chateau d'Hardricourt' in a suburb of Paris, 6 December 1984 Bokassa with some of his children at the chateau in 1984

The self-proclaimed Emperor of Central Africa had an estimated 50 children.
Source: BBC

3 comments:

Evarist Chahali said...

Muda wa kusoma wanao?Wako bize zaidi kutumia kila dakika ya uhai wao madarakani kutuadhibu kwa kuwachagua watuongoze.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kwa vile nilisoma UCLA, mitaa hiyo ya Malibu, Bell Air, Beverly Hills na Hollywood naifahamu vizuri sana. Huko Malibu kuna majumba ya kushangaza na watu wanamiliki fuko za bahari kiasi kwamba mlalahoi ukikatiza tu basi unakamatwa.

Ndiyo maana nilishangaa kidogo niliposoma makala katika gazeti la New York Times kuhusu hilo jumba la Teodoro Nguema Obiang (39) ambaye ni mtoto wa dikteta wa Equatorial Guinea - Teodoro Obiang Nguema Mbasogo. Mbali na hilo jumba lenye thamani ya dola 35,000,000 huyu kijana ana mali zifuatazo zinazojulikana hapa Marekani: Ndege yake binafsi – (dola 38,000,000), Magari manne aina ya Ferrari (dola 1,000,000), Rolls-Royce mbili (dola 700,000), Maybachs mbili (dola 700,000) na Bentley Arnage moja (dola 240,000). Isitoshe huja kupumzika Marekani zaidi ya mara tatu kila mwaka na kila anapokuja huja na pesa taslimu zisizopungua dola 1,000,000 kinyume na sheria za uhamiaji za Marekani.

Wakati huo huo wananchi wa Equatorial Guinea wanaishi katika umasikini wa kutupwa japo nchi yao ni mzalishaji wa tatu wa mafuta barani Afrika. Ndiyo maana nimekuwa nikisema kwamba matatizo yetu mengi sisi Waafrika ni ya kujitakia tu; na mengi yanasababishwa na uroho wa viongozi wetu kama huyu kijana asiyejali.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu huyu fisadi Teodoro Nguema Obiang (39) hapa:

http://matondo.blogspot.com/2009/11/kwa-ufisadi-kama-huu-afrika-tutaendelea.html

Uroho wa aina hii yaani mpaka unaumiza roho !!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mwl. Matondo nakushukuru sana kwa kuongeza data. Kuna haja ya kuwaandama hawa wezi hadi kieleweke. Kitu kizuri ni kwamba umeona hii kufuru kwa macho yako.Na hilo ni tone tu. Bado mali zilizoko kwenye beaches kama vile Ibiza, Hawaii na kwingineko.