How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday, 20 February 2011
Gadaffi anywea mwanae abwabwaja waandamanaji wazidi kupeta
Mtoto wa imla wa Libya, Al Islam Gadaffi kachafua hali ya hewa kwa kuongeza mafuta kwenye moto. Amelaumu jeshi kwa kutokuwa na viwango huku akikanusha mauaji ya wazi ya watu zaidi ya 172. Kijana ambaya hana mamlaka yoyote kisheria amebwabwaja hadi kuahidi kubadili bendera na wimbo wa taifa kama waandamanaji watapenda.
Kwa waliomtazama kwenye runinga wametoka na picha moja-Gadaffi kwisha kazi yake. Na inavyoonekana, haitachukua muda mrefu kama Misri au Tunisia. Wengi tumeshangaa mantiki ya kulaumu jeshi wakati bila jeshi hawa wezi hawana pa kushika. Mji wa Benghazi umeishakamatwa na waadamanaji na habari zaidi zinasema waandamanaji wanaelekea Tripoli kutoka miji ya jirani. Benghazi ni sherehe za kuanguka utawala dhalimu wa miaka 42 ya imla Gadaffi.
Mtoto wa Gadaffi akiwa amechanganyikiwa wazi, ametoa mpya kwa kusema eti waandamanaji wamefanya hivyo kutokana na kutumia mihadarati! Ni vituko vitupu. Tuzidi kuomba wimbi hili liendelee na kushuhudia kihiyo huyu akiondolewa kwa aibu zote. Wengi walizoea kumuona Gadaffi kama mtu jasiri. Kumbe, kama Saddam Hussein, ni hovyo tu! Kuna uvumi kuwa Gadaffi mwenyewe ameishakimbia nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Huu upepo wa mabadiliko unaishia huko juu kwa Waarabu tu ma unashuka Mashariki ya Afrika pia ambako unahitajika kwa hali ya juu?
Wimbi la mabadiliko ukanda wa Arabuni linasababisha viongozi wengi walale jicho moja wazi, "maluweluwe" wala siyo siri.
Da Subi nakubaliana nawe mia kwa mia. Hawa wezi na washenzi waliolewa madaraka hawana uwezo mkubwa wa kusoma alama za nyakati. Hata akina Dowans wetu bado wanafarijiana kuwa haya hayawahusu wakati yanawahusu sana kuliko hata hao akina Gadaffi. Kimsingi tunajifunza kitu kimoja-watawala wetu wala watu ni wababaishaji na woga wa ajabu wasio na mipango ya kesho zaidi ya ufisadi. Mungu tufungue macho tuwatolee uvivu kwa ajili ya vizazi vyetu vyenye heshima na si kondoo na walevi kama sisi.
Post a Comment