Najua wengi hapa wameishaanza kupiga
ramli kuwa huenda naongelea maeneo ya Beverly hills au New York kwa matajiri.
Kwa waliowahi kuishi New York watakuwa wanajua maeneo kama Westbury,
Brigdehampton, Sands Point na kwingineko ambako wenye nazo ima huishi au kwenda
kutanua hata kwa kufanya mambo ya kipuuzi.
Pia wapo wanaodhani kuwa napanga
kwenda kwa walevi wa Bongosalama kuwashitakia walioniibia kama siyo kutafuta
kuhurumiwa kwa uzembe na sababu ya kweli iliyosababisha nilizwe. Mmenoa!
Sikuibiwa New York wala siandiki kuomba kukutana na waze sorry walevi wa
Dalasalama.
Mwenzenu juzi nilitinga kule
Ngorongoro kwenye hoteli ambayo jina lake siri yangu kutanua na dogodogoz baada
ya kumuacha bi mkubwa solemba. Baada ya kuwa amenichosha kutokana
na kunenepeana ukiachia mbali kuwa bize kutumia nafasi yangu kutafuta ulaji
binafsi yeye na ndugu zake, nilijihisi kumchoka. Hivyo, niliamua kutafuta
vidosho lau nijiburudishe. Niliamua kwenda kufanyia ufuska wangu sehemu
iliyojificha ili asininase. Nilijua nimepata kumbe sikujua nilikuwa
nimepatikana. Nilijiona bonge ya mjanja nisijue mwisho wa yote nitaonekana fala
haswa! Uliwahi kusikia stori ya paka mrembo yaani mama anayerembua mimacho kama
hururaini la jamaa zangu fulani?
Baada ya kutinga zangu Ngorongoro
nikijifanya nilikuwa kule kikazi, niliingia mitaani kuwasaka ndogondogoz bila
kujua ni hatari. Ama kweli yule jamaa aliyeimba kuwa ndogondogo kwa pesa ni
hatari hakukosea hasa mwenye kuwa nazo anapokuwa kigogo kama mimi. Hivyo basi,
baada ya kutega nyavu zangu na kunasa kidosho cheupe, tuliamua kwenda zetu
chumbani kwangu kujivinjari. Tulijivinjari kweli kweli hadi nikachoka sana.
Kabla ya kulala tulipata kanywaji ili kuamsha mwenembago. Kumbe kale kanywaji
kalikuwa kamewekewa bwimbwi kiasi cha kunifanya nilale kama kichanga. nilipokuwa
nakoroma kama gogo, si dogodogo aliamka na kusanya kila nilichokuwa nacho
kuanzia laptop zangu nne, dolari 80,000 nilizokuwa nimehongwa na jamaa waliotaka
niwape tenda ya kusambaza kahawa kijiweni, madafu 20,000,000 ambayo yalitokana
na msaada wa shirika moja ambalo sitaki kulitaja na hata god father yangu yaani
pupi yangu. Nilipokagua vitu vyangu nilikuwa kuwa briefcases mbili zimekwenda,
Sanduku la silaha ya kujikinga na umeme au kondoo muu nalo limekwenda.
Inaonekana huyu manzi hataki kufa kwa miwaya. Yaani anaondoka hata zana zangu
ili nisiwanonihino wengine siyo?
God father imekwenda, suruali, viatu,
saa hata leso yangu vyote vimekwenda. Changu huyu alijua kukomba usiambiwe! Yote
tisa. Hivi bi mkubwa akiipata naye si ataamua kunikomoa kama hana akili nzuri?
Maana kwa mfumo dume huu tumekuwa kama vipofu bila kuangalia upande wa pili.
hivi bi wakubwa zetu wakiamua kulipiza kisasi kuna mtu atapona kweli?
Baada ya kugutuka na kujikuta mimi na
mashuka ya hoteli, nilipigwa na butwaa huku nikihisi kuchanganyikiwa jinsi
nitakavyotengeneza stori ya kusadikika kwa ndata. Unadhani bila kutengeneza
stori bi mkubwa angenielewa? Laiti angejua kilichosababisha nikwapuliwe wala
asingehangaika kunionea huruma bali kunikomoa. Kwa vile wakubwa huwa
hawaadhiriki, ilinibidi nicheze chess na ndata wambambikizie mzoba mmoja kesi
ili kuninusuru. Unacheza na uzito nini?
Unaweza kuamini kuwa kama changu
aliyeniliza angekuwa jambazi ningefungwa? Maana wakati akinisanya, nilikuwa
kulikuwa na bastola niliyokuwa nimeazima kwa jamaa yangu ili kujilinda. Pia
kulikuwa na SMG kali sana. Hamna haja ya kuanza kupiga ramli tena. Kinachoitwa
SMG siyo bali jambia la kimasai. Hata hiyo bastola si ya kweli bali toy lake.
Hayo tuyaache. Maana nisingeweza kuwa na bastola hata kama siku hizi ni ruksa
kuzinunua na kuzitumia utakavyo kama brother Dittope. Kwa mtu kama mimi SMG la
nini wakati mimi si jambazi? Hii imenikumbusha rafiki yangu mzee Headguard
Makorora Majogoo aliyesafiri na gobole lake toka Bongo hadi ugabacholini bila
kustukiwa. Walijisemea wahenga. Unaweza kumtoa mtu porini lakini huwezi kutoa
pori kichwani mwake. sasa mzito mzima na misilaha ya kivita ya nini? tena hali
inakuwa mbaya unapokuwa umebeba midude kama ile halafu ukajiingiza kwenye
uchangudoa na uhuni kama ilivyotokea. Licha ya kunitokea mimi, imetokea wapi?
Nachema chichemi njomba.
Pia mabingwa wa udaku nawashauri na
kuwaonya wasihusishe kisa changu na cha yule kijogoo mwana wa Milima ya Kigoma
aitwaye jina mumewe Eva. Yeye aliafanya uhuni watoto wa mjini wakamuingiza mjini
kikweli kweli. Kwanza mzito na SMG wapi na wapi kama siyo ulimbukeni na ushanba?
Wazito wanalindwa na bodigadi. Mi-SMG na mibastola ya nini kama siyo kuwa na
kazi zaidi ya moja? Maana bila kuwa na shughuli za siri mtu wa aina yake
asingeweza kujizungushia mizana mizito mizito kama Osama bin
Laana.
Turejee kwenye kisa changu. Kwa vile
huyu changu aliyeniibia amejifanya mjanja, basi ajue amejiharibia yeye na vyangu
wote wa kaya hii. Maana mwakani nitakapogombea uzito na kuupata nitakuwa
sichukui vyangu wanuka jasho wa kaya hii. Badala yake nitakuwa nachukua vikinda
vya shule au chuo na kwenda kutanua navyo majuu ambako siwezi kugutukiwa wala
kuibiwa. Ikizidi nitakuwa nachukua vyangu wa kizungu badala ya hivi vya
Kiswahili ambavyo vina shughuli zaidi ya moja; yaani uchangu na ujambazi.
Kuanzia leo natangaza rasmi. Changudoa yeyote atakayepita mbele yangu naramba
shaba au njaramba. Sina mchezo tena. Machangudoa wote wawe wa kisiasa au kingono
washindwe na kunyong’onyea. Na shetani aliyenishwawishi nikalala na changu
akaniibia naye ashindwe pamoja na changudoa wake.
Hivi hii ni kweli? Nimeinyaka kuwa
tangu jamaa alizwe kule kwenye mji karibu na bahari, vyangu sasa wanaipata fresh
hasa pale ndata wanapowasanya kulipiza kisasi kwa kuingizwa mjini bwana wao.
kuna mbea amenipa stori kuwa ndata nao wana lao. Maana wakiwakamata machangu
huwatoa mchicha hata huduma ya chap chap. Jamani, miwaya itatumaliza hata
tukijizungushia mipisto na miesmjii.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 21, 2012.
5 comments:
Duh! hii kali. Je ni mji karibu na bahari au mji kasoro bahari kama wasemavyo wenye? kama ni mji kasoro bahari basi ujumbe umefika.....
Bwana Malkiory umeanza nawe! Hapa ni mji ndani ya bahari ya milima. Upo hapo mshirika? Kazi kwao sisi tumemaliza.
Duh! nimeambulia surface meaning tu, lakini hidden meaning pengine inagusia moja kwa moja tukio la hivi karibuni la kule mji kasaro bahari.
Yote bado ni maana hujakosea.
Kaaz kwer kwer!
Post a Comment