How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday, 12 August 2012
Kurudi kwa Dk Ulimboka sawa je wabaya wake hawatammaliza?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Watanzania wapenda amani na haki walifurika kwa furaha kumlaki shujaa wao Dk Steven Ulimboka anayesemekana kutekwa, kuteswa na hatimaye kujaribu kuuawa na wale aliodai walitumwa na ikulu baada ya kuonekana kuwa mwiba kwa serikali wakati wa mgomo wa madaktari. Ingawa ni haki yake kurejea nchini, kuna haja ya kujiuliza maswali kidogo kuhusiana na hili. Je wabaya wake hawatataka kummaliza ili kukwepa kuumbuliwa? Je ana hakikisho gani la usalama? Je ni busara kurejea bila haki kutendeka? Kwa Tanzania ilivyogeuka nchi ya utawala wa hovyo, blog hii ina wasi wasi na usalama na maisha ya Ulimboka. Maana akina Ramadhan Ighodu na Jack Mughendi Zoka bado wapo na waliowatuma wapo na wanajulikana kwa kulipiza visasi. Time will surely tell.
1 comment:
hata wakimmaliza ukweli unajulikana,hao ccm cku zao zinahesabika hilo liko wazi check walivyong'aka kuona chadema imechangiwa na wananchi
Post a Comment