How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Sunday, 17 February 2013

Maskini Tanzania inaangamia hivi hivi!

Mauji ya padre Evarist Mushi na yale ya mchungaji  Matayo Kachila ni ushahidi kuwa ndoto ya amani na mshikamano inaanza kuyeyeka. Je ni kwanini watawala wetu wanafuga jini hili la udini wakati wakijua fika kuwa kama litapewa makazi hakuna atakayenusurika? Je tatizo ni kuwa na viongozi wadini au wasio  na visheni ya kuona mbali?
Ni ajabu kuwa alipouawa padre Mushi raisi Jakaya Kikwete alikaririwa akisema, "Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha mpendwa marehemu Padri Mushi na msiba huu ni wa kwetu sote," Kama rais maneno yake hayaingiii akilini. Badala ya kueleza atashughulikia vipi kadhia hii ya udini anajifanya kuwa pamoja na waombolezaji na wafiwa. Au anatimiza utani kuwa anapenda sana misiba? Sikuamini baada ya kusoma maneno ya Kikwete. Alipouawa mchungaji Kachila alisema wakristo watulie. Yaani watulie wamalizwe siyo? Tumwambie Kikwete ukweli bila woga amefuga udini kwa faida anazojua mwenyewe. Kwa mfano, ameelezwa kuwa chanzo cha yote haya ni mihadhara ya kidini inayoendeshwa na wachumia tumbo wasio na elimu hata ya dini yao. Hajaipiga marufuku. Ameelezwa kuwa kuna ajenda ya siri ya watu wanaodhani kuwa Tanzania inaweza kuendeshwa kiislam amenyamaza. Je kunani kama siyo kuwa mshirika wa nyuma ya pazia? Maskini Tanzania inaangamia hivi hivi. Maana siku hao wanaouawa wakiamua kulipiza kisasi na wanaweza kulipiza maana ni wanadamu. hakuna atakayenusurika. Nani ataendelea kuwa mpokeaji wa maiti ya ndugu zake wanaouawa bila kosa isipokuwa imani yao? Tufikie mahali tuangalia ukweli bila makengeza. Hata hao wakristo ni watu na wana hisia sawa na hao wanaowaua. Nisingependa tufike huko.
Kikwete acha usanii shughulikia matatizo ya udini vinginevyo nawe utaangamia baada ya kuiangamiza nchi.

3 comments:

Anonymous said...

"makengeza" yaani watu hawaoni kuwa hiyo madili ya wauzaji maunga?
wanamalizana wenyewe kwa wenyewe.
halafu watu wenye akili wanashupali kulipiza kisasi na wao wapo nje ya nchi.
halafu watatwambia ati kuna watu wanawafata wanataka kuwauwa kama chalali ni bangi tuu na ufikiri mfupi

Anonymous said...

drug delears hao wasichanganye mambo
fanyeni uchunguzi
nawe mwandishi unapurukuka una kiwewe?

Anonymous said...

Umesikia askofu shayo kasema nini
"Siwezi kuhusisha matukio haya na tafauti za dini kikrist na islam.
bali ni ukosefu wa umakini kwa watendeji wa vyombo vyenye dhamana ya kusimamia maisha ya watu.

"Bangi mtu huvuta akiwa ameshakula chakula halafu ndo anavuta Bangi"