The Chant of Savant

Tuesday 4 June 2013


Kurejea kwa mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)  Absalom Kibanda ni faraja na furaha na habari njema kwa waandishi wa habari. Kibanda ambaye alitekwa na kuumizwa vibaya hadi kunyofolewa kucha na kutobolewa jicho alikuwa nchini Afrika Kusini akitibiwa tangu alipofanyiwa unyama Machi 5. Kwa wanaojua roho mbaya na unyama vilivyolikumba taifa letu wanahoji kama kurudi kwa Kibanda ni jambo la busara au kujitoa kafara ili amalizwe vizuri kama kweli chanzo cha masahibu yake ni kazi yake na si mengineyo. Je nani amemshauri Kibanda kurejea nchini hata kabla ya uchunguzi wa masahibu yake haujakamilika? Je 'wabaya' wa Kibanda watakubali yaishe au watataka kummaliza ili siri yao isifichuke kama kweli chanzo cha masahibu yake ni kazi yake? Je kesi ya Kibanda itaishia kuwa kiini macho kama ya Dk Ulimboka ambaye ameacha maswali mengi kuliko majibu? Je ni kitu gani kimemmotisha Kibanda kujirejesha kwenye mikono ya mauti kirahisi hivi?
Ni mapema kuelezea. Wapo wasiomtakia mema wanamlaumu wakisema kuwa likimpata tena asilielie. Wanaompenda tunasema:  Alluta Contiunua. Tunachukua fursa hii kumtakia afya njema Kibanda na familia yake huku tukimpa pole kwa yote yaliyomsibu.

2 comments:

Anonymous said...

Kuna baadhi ya watu yani wanaacha kazi za muhimu kufanya ati anakwenda airport kumlaki kibanda ama kweli tumeishiwa mgelifunga basi hayo maduka hapo kariakoo ndo tungelijuwa kuwa mnampenda Kibonzo. yaani hao wote wamekosa kazi za kufanya kupoteza maasaa kibao airport ati kibonzo kaja sasa ndo iwe nini.

fanyeni kazi wacheni kusingizia kufanya mambo yasiokuwa na msingi na faida kwa taifa.

silaumu kuja kwa kibonzo nalaumu kwa nini asije jumapili ambapo watu wengi wanakuwa off ni siku ya mapumziko yaani mtu anamwaga bosi wake asubuhi anakwenda airport kumlaki kibonzo watanzania wana vichekesho kweli ninajie nchi gani imefanya uwoza kama huu

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo ni kweli ingawa suala la kufanya kazi au kutofanya kazi ni maamuzi ya wahusika binafsi. Kwa ufupi ni kwamba huu ni ushahidi kuwa taifa letu ni la wavivu wasiothamini kazi. Hebu tazama rais wetu anavyozurura kila uchao huku akiandamana na watu wengi wasio na umuhimu na kufanya shughuli zisizo na tija kwa taifa. Hiyo ndiyo nchi yetu iliyosalia.Tuikomboe toka kwenye mikono michafu ya wezi na wavivu.