The Chant of Savant

Tuesday 11 June 2013

Jeshi linaendelea kuiteka na kuitawala Tanzania

Habari kuwa aliyekuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  Ret. Leut. Gen Abdulrahaman Shimbo (anayekula kiapo kulia pichani) ameteuliwa balozi wa Tanzania nchini China ni matusi ya nguoni. Kumbe Shimbo alipokuwa akiitishia CHADEMA alikuwa akitumikia chama chake! Ni utapeli kiasi gani wakuu wa majeshi kuwa makada wa CCM? Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi za juu wa jeshi kuonyesha kuwa kada wa CCM. Alianza mkuu wa majeshi mstaafu aliyekuwa na kashfa nyingi za ufisadi Gen. Robert Mboma alipotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM wananchi wakambwaga. Alifuatia IGP mstaafu Omar Mahita ambaye kashfa ya kuzaa na mtumishi wa ndani ilimwacho hoi kisiasa. Sasa kuteliwa kwa Shimbo ni ushahidi kuwa Tanzania inatawaliwa kijeshi kichinichini. Ushahidi zaidi ni kujazana kwa wanajeshi kwenye nyadhifa tata za wakuu wa wilaya na mikoa na sasa kwenye balozi zetu. Hakika huu licha ya kuwa uzembe na uhovyo wa Kikwete ni ufisadi wa kimfumo. Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Tunalaani mchezo huu mchafu wa kujuana kulindana na kufadhiliana kwa kodi za wananchi.

No comments: