How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Monday, 10 June 2013
Rwanda wamefikia hapa?
Tanzania inaanza kuonja joto ya jiwe kwa kimbelembele chake. Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete alipayuka kuwa imla wa Rwanda Paul Kagame ajadiliane na waasi wa FDLR walioko kwenye misitu ya DRC. Rwanda kwa kutumia vyombo vyake vya habari hasa gazeti la New Times wameamua kumvua nguo Kikwete. Hiyo katuni ni ushahidi mmojawapo. Kwa wanaojua jinsi Tanzania ilivyochangia kuwaingiza akina Yoweri Museveni na Kagame madarakani wanashangaa kutenzwa hivi. Laiti Tanzania chini ya Ali Hassan Mwinyi wasingedanganywa na Museveni na kuruhusu ndege ya rais wa zamani wa Rwanda kutunguliwa tusingefikia hapa! Je Tanzania itajifunza au itaamua kuzifunza adabu tawala zilizotokana na kazi ya mikono yake? Tumefilisi nchi yetu tukimwonea Idd Amin ili kumuingiza Museveni na baadaye kushiriki kwenye jinai ya Rwanda kwa kuruhusu mkutano wa Arusha wa 'Amani' ufanyike huku tukijua fika yatakayojiri na sasa tunalipwa hivi!
Ajabu wachovu kama hawa ndio wanaotushawishi eti tuungane nao kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki wakati wana matatizo mia kidogo! Hawana ardhi, hawana demokrasia wala subira wa nini hawa? Siku zote tunasema heri tuungane na Zambia kuliko vijiinchi visivyo na kichwa wala miguu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment