The Chant of Savant

Friday 13 December 2013

Unajihisi vipi unapokuta kuwa taasisi yako ya umma imeajiri watu kidini au kikabila?




Tanzania ilisifika kuwa taifa lisilo la kikabila hata kidini. Watanzania tulizoea kuwacheka jirani zetu wa Kenya kwa kuendekeza ukabila. Tulizoea kuwashangaa wanigeria kwa kusumbuliwa na udini. Tulizoea kulaani jinai hizi. Ajabu ya maajabu ni kwamba kwa sasa Tanzania tunao udini na ukabila saa nyingine kuliko hata hao tuliozoea kuwacheka. Je unajisikiaje unapogundua kuwa taasisi inayoitwa yako na ya umma imeajiri watu wa dini au kabila moja simply because mkuu wa taasisi hiyo ni kutoka kabila au dini hiyo? Je tunao mawaziri na hata majaji wangapi wanaosemakana kuajiriwa kwa misingi ya udini au ukaribu wao kwa rais au mkewe? Shukuru Kawambwa, Adam Malima, Hawa Ghasia na wengine mnanipata? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

4 comments:

Anonymous said...

Kufilisika kimawazo kunachangia kujihalalisha kupitia imani na miujiza ili kupata washabiki wa wapiga kura mbumbumbu...na kuleta viongozi hovyo hovyo...watu hovyo hovyo tawala hovyo hovyo, maisha hovyo hovyo kila kitu shaghalabagala

anjela said...

Matokeo tunayaona kila siku inabidi baraza la mawaziri livunjwe.what a shame

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon, una usongo kweli kweli. Naona ufupisho wake umegusa karibu kila kitu. Asante sana kuliona hilo hivyo. Tuililie nchi yetu inayozidi kumezwa na kansa ya udini ukabila wizi ujambazi, ufisadi, uvujaji, uzururaji na hata kulindana.
Anjela nakubaliana nawe. Kila uchao tunaona vituko. Imefikia mahali eti tunaambiwa nyumba ya vyumba vitatu inauzwa dola laki moja na ushei tena kwa kutaka wanunuzi walipe kashi kana kwamba pesa inadondoka toka mitini. Huu ni ushahidi tosha wa taifa la kifisadi na kijambazi.

Anonymous said...

Nchi iliyofilisiwa na udugu na kujuana kama Tanzania, ina matumaini machache sana ya kusonga mbele. Hata hivyo nafasi ipo. Kwani kama tunaona kuwa makamba alishindwa January ataweza kweli? nAPATA SHIDA hapa. Labda tukate matawi, yaani tuondoe majina ya Mwinyi, Kikwete, Wasira yaani tuanze upya! Lakini inawezekana? Hapana, lazima tukate mzizi tena tusiishie hapo tu, tukusanye mabaki yake yote kisha tuchome moto.