Saturday, 8 October 2016

Kumbe 'usanii' unalipa!

Angalia babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapila anavyoonekana kabla ya kuibuka na baada ya kuzinyaka akiwahadaa wajinga kuwa ana tiba ya ajabu wakati alichokuwa nacho ni uongo wa ajabu. Je namna hii mfumo wetu haujaruhusu jinai ya kuibia maskini na wenye shida kwa manufaa binafsi. Ingekuwa Ulaya wala huyu tapeli asingefanikiwa. Maana angetakiwa athibitishe tiba yake kimaabara. Ama kweli wajinga ndiyo waliwao!

No comments: