The Chant of Savant

Wednesday 1 December 2010

Pigo kwa kitabu cha NYUMA YA PAZIA




Wapendwa wasomaji,
Naandika taarifa hii kwa imani kuwa tutasaidiana hata kukwamuana tokana na mkwamo huu. Nafanya hivyo kwa imani moja kuwa tutasaidiana na kushinda. Mficha maradhi kilio humfichua na mficha uchi hazai.

Niliwataarifuni siku za nyuma kidogo kuwa nilikuwa nikitegemea kutoa kitabu kingine baada ya kile cha SAA YA UKOMBOZI ambacho si haba kinafanya vizuri kwenye soko. Tuliingia makubaliano ya awali na mchapishaji ambaye alinipa moyo kuwa angekichapisha tena haraka kutokana na uzuri wake.
Nilisanifu jarada na kukamilisha kila kilichonipasa ikabaki uhakiki ambapo- kama alivyokuwa ameniarifi-walikuwa wakiondoa au kutafsiri maneno ya kimombo. Lakini baada ya kupeleka mswada kwa wahakiki wake(kama alivyonieleza baadaye) alikuja na jibu la kustua kidogo. Alidai kitabu tajwa kinamlenga mwanasiasa mmoja ambaye naomba nisimtaje jina. Mwanasiasa aliyedhaniwa kulengwa na kitabu hicho aliwahi kushika madaraka makubwa nchini mwetu lakini tokana na kutoyamudu vizuri au tuseme kuyatumia vibaya kwa faida binafsi, alitimliwa.

Hivyo, mchapishaji alikiona kitabu tajwa kama shambulio kwa mtu huyu maarufu ingawa si lengo la kitabu husika. Hata kwenye barua yake ya kunijulisha kusitisha kuchapisha kitabu alisema anaogopa ila kitabu ni kizuri. Hivyo nitafute mchapishaji mwingine.

Hivyo basi, nimeona niwasiliane na wasomaji lau nipate ushauri hata msaada wa kuchapisha ikiwa ni pamoja na kuwajulisha kuhusu kuchelewa kutoka kwa kitabu. Naamini hivi kutokana na blogu hii kusomwa na watu wa rika na kada zote.

Hivyo, kwa ufupi na majonzi, ni kwamba kitabu cha NYUMA YA PAZIA hakitatokea mapema kama kilivyotarajiwa kutokana sababu hiyo hapo juu. Kitabu hiki sikisifii kinajadili mambo mengi hasa kubwa likiwa ufisadi, jinsi wakubwa wanavyoibia umma nyuma ya pazia na maskini wa kutengenezwa kuwaua wenzao huku wakiwaogopa mafisadi. Kitabu hiki ni magnum opus kusema ukweli.

Katika hili nimejifunza kitu kimoja-jamii yetu ina miungu watu wasiopaswa kuguswa wala kukosolewa. Wana macho na masikio kila mahali. Je namna hii hatuufanyii ujuzi na akili ufisadi jambo ambalo licha ya kuwa la aibu na ajali ni balaa kwa jamii yetu inayoanza kubobea kwenye ibada za watu na vitu badala ya ukombozi na haki? Je tumekubali kujirahisi hivi ili tuwe sababu ya kuangamia kwetu huku tukiwa mashahidi wa angamio na pigo hili? Je tugwaye na kunung'unika au tuzidi kuwapa hard time hadi kieleweke.
Naomba maoni yenu.

11 comments:

Mbele said...

Yawezekana utapata ushauri bora zaidi kutoka kwa wengine, lakini nami napenda kukushauri kwa namna yangu.

Tekinolojia ya uchapishaji inasonga mbele muda wote, nami kwa miaka kadhaa nimekuwa nikifuatilia, na hatimaye nikaanza kuchapisha vitabu vyangu kwa kutumia tekinolojia hii ambayo inakuwezesha kiurahisi kabisa kujichapishia vitabu wewe mwenyewe bila kuwategemea wachapishaji kama tulivyozoea.

Nimeandika kuhusu jambo hilo katika kitabu cha CHANGAMOTO.

Kutokana na uzoefu wangu, nimewasaidia watu kutoka Caribbean, Marekani, Nigeria na Tanzania kuchapisha vitabu vyao kwa mtindo huu.

Ushauri huu natoa bure. Najiongezea uzoefu, ambao utanisaidia huko mbele ya safari, nitakapostaafu kazi ya darasani. Hapo nitaanza kuwatoza wateja wa huduma hii, ili angalau nipate vihela vya sabuni na kabia kamoja. Nadhani tunakubaliana kuwa huu utakuwa si ufisadi, hasa ukizingatia kuwa walalahoi nitakuwa siwatozi chochote :-)

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka Mbele,
Shukrani kwa mara nyingine kujitokeza kunisaidia. Nitafanya hivyo kuhakikisha kuwa hatuzibwi midomo kutokana mafisadi kutandawaa nchi nzima. Watuzuia kuchapisha kwa kutumia wachapishaji lakini siyo sisi wenyewe kufanya hivyo. Baada ya kupokea kitabu toka kwako nadhani tutawasiliana zaidi kuona pa kuanzia na kuishia. Kila la heri na asante kwa mara nyingine kwa mchango wako wenye afya.
Kutowatoza walalahoi chochote ni mchango mkubwa sana kwa bongo zetu zilizolemazwa na mawazo mgando na utawala mfu na mchafu.

Mbele said...

Hakuna tatizo, tutawasiliana hata kwa barua pepe. Anwani yangu ni info@africonexion.com

Makala moja niliyowahi kuandika nikigusia suala hili ni hii hapa.

Anonymous said...

Kweli hali ni mbaya sana. Nimesoma na Raia Mwema imefanyiwa kitu mbaya kama wewe!
Kweli tumekubali kukamatwa mateka tukiona. Something must be done. Now now and now!

Anonymous said...

Mimi hiyo kava tu ya behind the curtains na huyo fisi anayechekelea ndo wamenomaliza kabisa, i just cant wait for the book!

Anonymous said...

Hiyo chata inatisha. Kama ndiyo huyo Lowassa, basi kazi anayo tena kubwa.
Chapisha hilo chata watu tusome na kufaidi mwaego.

Simon Kitururu said...

Kazi ipo! Nilichotaka kusema naona Prof Mbele ndiye Mtaalamu!

Lakini nahisi hivi karibuni tutajiwezesha tu wenyewe bila vitisho kwa kuwa katika jamii yetu BONGO sasa hivi kama wewe sio mtu wa YES MAN au tu wale watiio falsafa iitwayo kifundisho ``Usijifanye mjanja na unajua kama unataka KULA NA VIPOFU´´ kama nilivyostuliwa mahali ,.... utakwepwa kwa kuwa kwa wengi wenye nguvu TANZANIA ,...

kwao VIPOFU ni muhimu -na hapa siongelei vipofu wenye ulemavu wa macho.:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mwalimu Mhango;

Usikate tamaa. Tamthiliya ya Kaptula la Marx ya Euphrase Kezilahabi ilichukua miaka mingi sana kuchapishwa na ilisemekana ni kutokana na ukweli kwamba ilikuwa inamwandama kiongozi fulani. Lakini hatimaye iliweza kuchapishwa baada ya hali kupoa kwa kiongozi mwandamwa kumaliza muda wake.

Kama alivyosema Profesa Mbele unaweza kichapicha riwaya yako mtandaoni kwa sasa na mambo yakipoa unaichapisha "duniani". Au unaweza kujaribu kuitafutia mchapishaji ambaye yuko huru na ambaye hatishwi.

Pole kwa misukosuko!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nawashukuruni nyote mliotokea kunipa ushauri. Nitaufanyia kazi. Anonymous wa mwisho uliyemtaja siye wala hakuna mwanasiasa aliyelengwa zaidi ya kuwa hali halisi.
Anonymous first and second shukrani sana kwa uchungu mlio nao kwa nchi yenu.
Nzuzullima nakushukuru pia kwa kunipa moyo na mfano wa Kaptula la Marx. Hii nadhani niite kaptula la fisadi.
Kwa ufupi nimefarijika na michango yenu bila kusahau ule wa Mtakatifu mwenzangu Kitururu.

Anonymous said...

Halafu wewe Mkwazi unajifanya una uchungu na nchi yetu. Kama ni kweli kwanini unaishi ugenini? Usidanganye watu Lowassa ni mzalendo wa kupigiwa mfano. Kama wewe si fisadi unaweza kueleza ulivyoweza kwenda kuishi ugenini? Inaonekana unatumiwa na maadui wa taifa na bado ni kijana mdogo. Tunakujua. Nimesoma utumbo wako wa saa ya ukombozi. Hvyo kabisa hamna kitu bali chuki na uchochezi. Kama wewe mwanaume kweli chapisha hicho kitabu chako ndipo utaona kilichomtoa nyoka pangoni.
KWanza watanzania si wasomaji wa utumbo kama huu. Hata picha ya kitabu chako inaonyesha chuki tupu. Kila siku Lowassa wewe baba yako amelifanyia nini taifa zaidi ya kuzaa taahira? Sasa tia akilini. Utapotezwa kabla ya wakati wako.

Anonymous said...

Mchangiaji hapo juu si mstaarabu. Mambo ya kutishana yamepitwa na wakati. Kufa ni ada hivyo Mpayukaji usitishike na najua hutatishika. Alaaniwe awatishieaye wenzake wanapodai haki. Sitaki niandike matusi kwenye blogu hii vinginevyo ningesema kutishana ni use...
Kutishana ni dalili tosha za kushindwa. Tunawangoja hiyo 2015 inayowahangaisha. Mpayukaji kaza buti.