How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 31 December 2010

SALAMU ZA MWAKA MPYA



Nikiwa mpambanaji, kwanza, namshukuru Mungu kuniwezesha kuumaliza mwaka. Pili nawashukuru wasomaji wangu walionipa changamoto mbali mbali. Tatu natoa maazimio yangu ya mwaka tunaouanza.

Nina maazimio na malengo mengi binafsi. Lakini mawili si ya binafsi. Kwanza, nitaendelea kupambana na ufisadi kwa ukali zaidi.
Pili, nitawekeza kwa nguvu, sawa na kwenye ufisadi, kupigania KATIBA MPYA ili kuhakikisha jinai zilizotamalaki hasa ufisadi, uchakachuaji na ubabaishaji vinatoweka na taifa letu kusonga mbele.

Azimio la tatu ni kuhakikisha kazi zangu, yaani miswada, ambazo hazijachapishwa kuwa vitabu, inachapishwa.
Nina viporo kama vile NYUMA YA PAZIA, WAZALENDO WA DANGANYIKA, BUSARA, KILIO CHA MSIKWAO na VISA VYA MPAYUKAJI.

NAWATAKIENI HERI YA MWAKA MPYA KWA NIABA YANGU NA FAMILIA YANGU.
,

8 comments:

malkiory said...

Heri na kwako pia wewe na familia yako.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bwana Malkiory shukrani sana kunitakia heri ya mwaka mpya. Nami kama ada, nakutakia mwaka mpya wenye kila fanaka siha na utulivu wewe na familia yako. Tuombeane uzima na mafanikio hasa katika harakati zetu za kupambana na ufisadi na kudai katiba mpya.

Yasinta Ngonyani said...

Nami pia na familia yangu twawatakieni Kheri na fanaka kwa mwaka mpya 2011!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow! Da Yacinta asante sana kwa heri zako. Nami pokea zangu na familia. Naamini tutaliendeleza mwaka 2011 kwa nguvu na ukali zaidi.
God bless you.

Anonymous said...

Heri kwako pia kaka..Mwenyezi Mungu akuzidishie ufahamu na uzidi kuendelea kufichua maovu ya wanafiki wanaoharibu nchi yetu.

Anonymous said...

Kaka punguza wese maana naona unazidi kuharibika. Naona mambo supa kwa sana bro.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hebu basi hayo malengo yako na yakatimie. Kila la heri kwako na familia yako yote.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nawashukuruni nyote kwa dua na changamoto zenu.Nafarijika kuwa azimio langu la pili-katiba mpya, limepata jibu la awali.
HERI YA MWAKA MPYA 2011.