Sunday, 9 December 2012

Nchi ya matapeli na vihiyo: naililia Tanzania.

Kwa wanaomjua balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorous Kamala wanamjua kama mtu mwenye shahada ya juu Phd hivyo siku zote humuita Dk Kamala. Na hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi tangu akiwa mbunge miaka iliyopita. Ajabu eti leo ndiyo anatunukiwa hiyo PhD! Hii maana yake ni kwamba alijipachika cheo cha udaktari akalipwa mshahara wa kiwango hicho wakati hakuwa na sifa. Hili ni kosa la  jinai kisheria. Pamoja na kujulikana kwa ushahidi huu bado rais alimteua kuwa balozi nchini Ubelgiji. Je hapa rais wetu hajashirikiana na waharifu kuhujumu nchi yetu? Kesho utasikia akina Makongoro Mahangaa, Didace Masaburi, Matayo Matayo, Emanuel Nchimbi na Mary Nagu wakitunukiwa PhDs wakati waliishajulikana kama madaktari wakati si kweli.

1 comment:

Jaribu said...

JK mwenyewe ni tapeli na kihiyo, kuanzia hiyo JK.