Watanzania Watakiwa Kujenga Utamaduni Wa Kujisomea Vitabu
Wengi wanajiuliza kwanini yeye haonyeshi mfano na badala yake anatumia muda mwingi kuzurura na mumewe? Kwanini hamshauri mmewe kuwafukuza mawaziri na watendaji wengi aliowateua wanaojulikana kughushi vyeti vya shahada? Je yeye ukiachia mbali kutumia WAMA kujipatia pesa amefanya nini binafsi kuongeza kiwango chake cha elimu?
Na: Heka Wanna na Shakila
Galus,MAELEZO
MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma Kikwete wito kwa wananchi
tabia ya kujisomea vitambu na machapisho mbalimbali ili kujiongezea maarifa
yatakayowawezesha kujiletea maendeleo.
Mama Kikwete alitoa kauli hiyo kwenye Makumbusho ya
Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa makatba kwa ajili ya
watoto na watu wazima.
Alisema kuwa elimu ndio silaha pekee ya kukabiliana na
maadui watu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini na hivyo kujiletea
maendeleo.
Mama Kikwete aliongezea mbinu za kujiendeleza kimaisha
zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia vitabu na machapisho mbalimbali
yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na nje ya
Tanzania.
Alisema kuwa hiyo itasaidia katika kuongeza maarifa
kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo ya mawasiliano ambayo itawawezesha
watumiaji kupata elimu ya taaluma mbalimbali.
Aidha Mama Kikwete aliwasihi watumishi wa Makumbusho
hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili isaidie kukidhi malengo ya
kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora za kudhibiti matumizi yasiyo na tija
ya maktaba ikiwemo upotevu machapisho na vitabu mbalimbali na uhalibifu wa
vitabu unaofanywa na watu wasiotaka maendeleo.
Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru Balozi wa Korea Kusini
Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake kwa msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali
kwa ajili ya maktaba hizo mbili .
Chanzo: Mjengwa Blog.
No comments:
Post a Comment