Saturday, 29 December 2012

Unafiki na ujambazi wa waingereza

Bila aibu yoyote nchi za   Magharibi haziachi kuwalaumu majambazi zilizowatengeneza kuibia Afrika. Tuna majambazi kama Jomo Kenyatta, Mobutu Seseseko, Jean-Bedel Bokassa, Felix-Heuphet Boigny, Moise Kasavubu na wengine wengi waliotengenezwa na mataifa ya magharibi na kuigeuza Afrika shamba la bibi.

Ni bahati mbaya kuwa hata baadhi ya vibaka hawa kufa au kuondolewa madarakani, Afrika imezalisha vibaka wengine wa kizazi hiki. Leo wakati tukimaliza mwaka tumeona lau tulete baadhi ya sura za unafiki na ujambazi wa mataifa ya magharibi yakiongozwa na mama yao Uingereza.


No comments: