


Kipanya wakati mwingine hupayuka kwelikweli kiasi cha kuacha watu wakijicheka wakidhani wanawacheka wengine. Sijui kama bwana Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wanasoma au kusomewa darasa hili la Kipanya.
Today I’m going
to talk about my trip to the city of AR not Beijing. For those not well-versed
with what AR is, it is the city that became famous for two, or three, wrong
reasons. First, it is famous for producing Hunknite aka Bongonite
aka Tanzianite that’s made some neighbouring and distant countries richer
than it’s made us. Hunknite is the type of precious metal that is found
only in our hunk the world over.




Kama sanani zetu zina thamani, kwanini wakubwa wanapenda kununua samani nje? Hapo juu rais Jakaya Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la kiswahili rais wa seneti ya Ufaransa, Jean-Pierre Bel huko Paris hivi karibuni. Kujua huu ulivyo unafiki GONGA hapa uone inachofanya serikali ya huyu huyu anayejifanya kutangaza samani zetu wakati serikali yake inanunua samani nje kwa bei mbaya.

Hakuna asiyefahamu kukwa taifa la Misri haliwezi kuwepo bila mto Nile ambao hupitia Tanzania na kupata maji mengi toka Ziwa Nyanza. Hivyo, huwa hawapendi tutumie maji ya mto huu hata Ziwa Nyanza kwa umwagiliaji kwa vile tutapunguza kiasi cha maji wanayopata. Kutufumba macho, wamekuwa mstari wa mbele eti kusaidia miradi ya kijima ya kuchimba visima vya maji kwa watanzania ili kutuzuga tusielekeze maji ya mto Nile kwenye maeneo kavu. Kwenye picha waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe akikenua wakati wa kukata utepe wa uzinduzi wa visima 30 vilivyofadhiriwa na serikali ya Misri. Kushoto kwake ni waziri wa Umwagiliaji wa Misri Prof. Mohamed Bahaa el-Din Ahmed. Kweli tunapenda sana ufadhili hata kwenye vitu vya kijinga.! Kama mbwa, tunapewa fupa kuruhusu mwizi aibe ng'ombe.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa jezi ya mpira wa kikapu. Chini ni Rahma Kharoos akikabidhiwa jezi ya Simba huko Oman. Naomba usiniulize uhusiano wa marais hawa wawili. Mmoja ni rais wa nchi na mwingine ni rais wa kampuni ya mafuta ambayo iliibuka baada ya Kikwete kuingia madarakani. Wanahusiana vipi? Please don't ask me.
Tukisema kuwa utawala wa Kikwete ni wa kifamilia au ufalme fulani kama siyo usultani tunaambiwa chuki. Tusaidiane. Huyu mama hapa anapokelewa kwa ma rais kwa itifaki ipi kama siyo matumizi mabaya ya madaraka? Ni ajabu hata washauri wa mumewe hawalioni hili na kama wanaliona wanaoogopa kusema ukweli wasiteme kitumbua. Jamani it is too much. Ajabu wanajeshi kama hawa wakipiga picha na wapinzani wanaambiwa ni makosa. Ni vigumu kujua rais na mkewe nani ni rais katika hali hii na matumizi mabovu ya madaraka ya namna hii.
|
Ya kule mwisho wa
reli tuliyasikia ndata wawili walipomdedisha mlevi mmoja. Kisa?
Alikuwa anawadai uchache. Badala ya kumlipa vijisenti walimlipa kipigo
kilichomnyotoa roho. Kumbe akina Kamuhaanda wako wengi siyo?
Kwanza, ngoja nimlilie kidogo Daud Mwangosi aliyenyotolewa
roho na akina Kamuhaaanda. Ee mwenyezi Mungu nilipizie kisasi kwa mabazazi
wanaonyotoa roho za waja wako wasio na makosa.
Tuendelee. Juzi
nilinyaka habari kuwa walevi wameanza kuwachoma moto ndata baada ya kugeuka
vibaka, majambazi na majangili. Rafiki yangu aliyeko kule Ngala alinitumia
mikanda miwili jinsi ya ndata walivyonyotolewa roho baada ya kumnyotoa rho mlevi
mmoja huku wengine wakiuawa kule Nk’aagwe baada ya kutaka kudhulumu vipusa.
Ni ajabu kusikia
kuwa kumbe hata ndata wanafanya biashara ya pembe za ndovu! Kama hili ni hivi
jamani nani anatawanusuru hawa wajomba zetu—tembo? Walevi tulizoea kuwaona ndata
wakiwatoa kitu kidogo na kitu kikubwa wauza gongo. Baada ya kuanza biashara ya
mibwimbwi hasa ilipoanza kuwahusisha wanono, wanene na wazito, tulishuhudia
ndata nao wakipata chao kwa kuwatoza ushuru wauza bwimbwi. Anayebisha aende
mitaa ya Mnazi Mmoja aone jinsi wale wamama wanaouza mibwimbwi wanavyokata
ka-laki kila afendi akibisha hodi mlangoni. Asiyejua chesi zima ni kwamba baada
ya ndata kugundua kuwa wadingi wao wanahusika na mibwimbwi nao wakaona wajiweke
karibu na wauzaji huku wakiachia miteja iteketee.
Kama ndata na
wadingi wao wasingekuwa washirika wa biashara hii, unadhani ungeona teja hata
moja mitaani likitanua na kutanuka? Unajua siri ya Mkulu kusema kuwa ana orodha
ya vigogo wa mibwimbwi? Kwa taarifa yenu Njaa Kaya alichosema kuwa anawajua
wauza bwimbwi na ana orodha yao si uongo wala usanii. Kwa taarifa yenu mimi
ndiye nilimpa ile orodha. Nilimpa lini na wapi? Msiniulize kwani sitaki umbea na
isitoshe hii ni kile ambacho wataalamu huita top secret ya confindential. Are
you there dudes? Mdingi knows everything and he monitors almost every move to
see to it that he is not suffering any loss.
Samahani. Nimenogewa na
kikameruni nikasahau kuwa siyo lugha ya kaya ya taifa. Anyways, ninachotaka
kusema ni kwamba hata huu ujangili na ujambazi wa ndata msidhani ni jambo la
kuzuka tu. Umekuwapo muda mrefu. Jamaa yangu anayefanya kazi kwenye mbuga za
wanyama tangu enzi za Ruksa na Ndongara Muhunidini anasema kuwa kama walevi
wangejua kinachoendelea kule huenda wangejinyotoa roho kwenye kile ambacho
kingeitwa mass suicide au kujinyotoa roho kwa halaiki. Kwa wale ambao walikuwa
bado makinda ni kwamba genge la Ruksa na Muhunidini ndilo lililomnyotoa roho
mwandishi Stan Katabaro aliposhupalia ujambazi na ujangili wao. Nani
mara hii kasahau majina kama Brigedia Ali na Ortello Business Coop yaliyovuma
wakati wa utawala wa Ruxa? Nani hajui kuwa usafirishaji wa wanyama na nyara za
kaya unafanywa chini ya ushirikiano wa ndata na idara za mipakani na forodha?
Shauri yenu nyie endeleeni kudanganywa huku mkiliwa.
Tangu wakati ule
wanyama wameendelea kuuawa huku baadhi ya majambazi na majangili wenye madaraka
wakizidi kuneemeka. Waulize akina Pio Msekua, Khatiiib, Menghjii,
Lazaro Nyalando, Eze Maige na wengine wenye ulaji wao kule maporini. Wanyama
wanauawa ukiachia mbali kusafirishwa nje. Najua wengi watasema nachonga
nikimaanisha wale wanyama waliouzwa na yule habith wa kihindi Umangani kupitia
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mkia. Hao ni cha mtoto. Kuna wanyama ambao kwa
kitaalamu tunawaita exotic ambao wanauzwa kimya kimya bila walevi kujua. Hivi
mnajua kuwa kenge, nyoka, kobe, mijusi hata nguchiro ni big deal kwenye baadhi
ya nchi? Shauri yenu. Mkiona watu wanaukata na kuula mnadhani ni ngekewa msijue
kumbe wanawaibieni. Hebu angalia viwanja vilivyoota mbawa. Ukigusa kijiwanja
tena uchochoroni uswazi uaambiwa milioni hamsini! Bado hujajenga. Wenzenu
wanaangusha mije ngo ya kutisha nyinyi mnapanga mbavu za dog.
Ukiona akina Eze
Maige na Lazaro Nyalando wanaangusha mihekalu unadhani njuluku wamepata wapi
kama siyo kwenye ujangili na ujambazi huu? Hata hao ndata unaoona wanavaa buti
zilinazotembea soli upande usidhani ni walalahoi kama wewe. Ni matajiri wa
kutupwa. Wanafanya usanii kujificha nyuma ya uchovu lakini ukweli ni kwamba si
wachovu kama wanavyoonekana. Hii Danganyika na Danganyana bwana. Unaweza kuona
njemba ikifanya kazi ya kichovu yenye mshahara kiduchu lakini ikaangusha hekalu
la mabilioni na kumilki migari ya bei mbaya ubaki kushangaa. Wapo wengi sana
kiasi cha kugeuza kaya kuwa kaya ya majambazi na majangili. Nani aulize wakati
ujanja kupata hata kama kwa kushikishwa ukuta?
Kaya yetu imegeuka
ya majangili kuanzia juu kwenda chini. Kila mtu anajitahidi kuwa
jangili iwe ni kwa kuuza wanyama, watu hata kujiuza yeye mwenyewe hasa wale wa
kiwango cha chini kama watoto wa shule. Unashangaa kuona kibinti cha shule
kinamilki simu ya bei mbaya huku kikiwa na credit muda wote. Je kinafanya kazi
gani ya kukipatia kipato kama siyo kufanya ujambazi na ujangili wa kujiuza?
Hayo tuyaache.
Nani mara hii
kasahau nyara zilizowahi kukamatwa sehemu mbalimbali za kaya tena zikiwa ima
zimepakiwa kwenye magari ya sirikali au ndata? Nani mara hii kasahau sakata la
kukamatwa kwa maafisa wawili ndata huko Mugumu waliokuwa wakitokea Biharamulo
mnamo tarehe 5 Januari 2013? Mbona hata majina yao yanajulikana kuwa ni Kulwa na
Nyarata?
Funga kazi ni
ujambazii uliotokea hivi karibuni kwenye jiji la walevi la Dar –alaa-si-Salama
maeneo ya Msimbazii. Wajue nini kilitokea? Si majambazi yalikuja kwenye kituo
cha kuuzia wese baada ya kupewa inshu na wahudumu wa ndani kuwa kutakuwa na
mshiko ukisafirishwa benki. Wazee wa kazi walipoingizana na kuishia na madafu
kama vimilioni 150, si kikanuka hadi ndata kuingilia. Wacha shaba zitembezwe
mbichi mbichi. Walevi walidhani jamaa walikuwa wamekuja kuokoa zile njuluku
wasijue kuwa ndata nao walikuwa na lao. Si baada ya kuwazidi nguvu majambazii
wenzao ndata wakaishia na zile njuluku. Hadi leo naambiwa eti ndata watano wako
lupango kwa kushukiwa kuiba njuluku zile. Je hawa ni ndata au majambazi
tu?
Acha mie niende
kujililia. Maana ndata wanapogeuka majambazi na majangili waweza hata kuuza
vichwa vya watu hasa zeruzeru.
Eti gongo ni pombe?
Kwaheri!
Chanzo: Tanzania Daima Januari 16, 2013.
|
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alinusirika kipigo kutokana na kuingia kichwa kichwa kwenye sakata la gesi Mtwara. Akiwa Mtwara Mbatia aliyeandamana na wabunge wake toka Kasulu alisema maneno ambayo hayakuwafurahisha wadau wa sakata la gesi kuhamishiwa Dar Es Salaam. Kikubwa kilichomponza ni ile hali ya kuteuliwa na Jakaya Kikwete kuwa mbunge. Hivyo kwa akina njomba Mbatia si mtu wa kuweza kupingana na mtu aliyempa ulaji yaani Kikwete ambaye anaonekana kutaka miundombinu ya kusafirisha gesi iwekwe Dar na Bagamoyo kwa faida zake binafsi. Kwa habari zaidi GONGA hapa.


