Saturday, 19 January 2013

Kikwete kuficha majina ya ujumbe wake inaashiria nini?

Hakuna kitu kinawachanganya watanzania wengi kama tabia ya rais Jakaya Kikwete kwanza kupenda 
 uzurura nje. Na pili ni ile hali ya kuficha majina ya watu anaoandamana nao huko kwenye utalii wake. Leo hii tunaambiwa yuko Ufaranasa kwa ziara ya kikazi. Kaandamana na nani zaidi ya mkewe? Top secret. Je kuna watu wasiotakiwa anaoandamana nao wanaokula kodi yetu bila sababu? Maana tulizoea kusoma  majina ya watu wanaoandamana na rais kila aendapo tangia enzi za Nyerere,Mwinyi hadi Mkapa. Baada ya Kikwete kuingia na utawala wake wa kishikaji ni vigumu kujua majina ya watu anaoandamana nao na idadi yao. Jambo ambalo laweza kuashiria ufisadi fulani.

No comments: